Mkufunzi wa Chuo Afikishwa Mahakamani “Kaomba Rushwa ya Ngono”

Mhadhiri wa Chuo cha Taifa cha Usafirishaji,(NIT), Samsoni Mahimbo (68), amefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu akikabiliwa na kesi ya kuomba rushwa ya ngono kwa mwanafunzi wake ili amfaulishe katika mitihani wa marudio.

Mshtakiwa anadaiwa ametenda kosa hilo Januari 12 , 2017 huko katika nyumba ya kulala wageni ya Camp David iliyoko Mlalakuwa Mwenge.

Inadaiwa siku ya tukio, mshtakiwa akiwa muajiriwa wa chuo hicho cha NIT kama Mhadhiri kwa muhula wa kwanza wa masomo wa mwaka 2015/2016 wa somo la usimamizi wa barabara na usafirishaji (road transport management), lenye kodi namba 07101 alitumia mamlaka yake kutokana na nafasi yake chuoni hapo na kuomba rushwa ya ngono kutoka kwa mwanafunzi, Victoria Faustine ambae ni mwanafunzi wa chuo hicho anayosomea mafunzo hayo ya road transport management.

Inadaiwakuwa, mshtakiwa aliomba rushwa hiyo kama sharti kwa mwanafunzi huyo kuwa atamfaulisha katika mtihani wa marudio (Supplement) wa somo hilo uliokuwa ukifanyika January 5, 2017.

Hata hivyo mshtakiwa amekana kutenda kosa hilo ambapo ameachiwa kwa dhamana baada ya kutimiza masharti ya kuwa na mdhamini mmoja atakayesaini bondi ya Sh. Milioni 4.

Kwa mujibu wa upande wa mashtaka upelelezi katika kesi hiyo umekamilika. Kesi hiyo imeahirishwa hadi Septemba 17,2019 mshtakiwa atakaposomewa maelezo ya awali.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad