MKUTANO SADC : Magufuli atoa agizo la Zimbabwe


Mwenyekiti mpya wa Jumuiya ya SADC Dkt John Pombe Magufuli ameziomba Jumuiya za Kimataifa kuiodolewa vikwazo vya kiuchumi, Zimbabwe kwa kile alichokisema kufungiwa kwa nchi hiyo wanaoathirika hadi wanachama wa Jumuiya hiyo.


Rais Magufuli ametoa kauli hiyo jijini Dar es salaam wakati wa mkutano wa 39 wa SADC katika ukumbi wa Kimataifa wa Mwalimu Nyerere, ambapo aliwaomba wanajumuiya kulisema suala hilo.

"Zimbabwe wamekuwa kwenye vikwazo kwa muda mrefu, hichi kifungo tunaathirika sisi wote, napenda kupendekeza kupitia mkutano huu kuziomba Jumuiya za Kimataifa ziiondolee vikwazo Zimbabwe, na nawaomba wanachama wote tulisemee hili." amesema Rais Magufuli

Aidha kuhusiana na suala uchumi Rais Magufuli amesema "kwa mawazo yangu binafsi, nadhani kama tukifanya kazi kwa pamoja kama Jumuiya ya SADC, nadhani uchumi utakua zaidi ya asilimia 3.1."


Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad