Mlipuko Wauwa Watu 17 Mjini Cairo

Wizara ya afya ya Misri imesema mapema leo kuwa watu kumi na saba wamefariki dunia na wengine thelathini na mbili kujeruhiwa baada ya kutokea kwa mripuko nje ya Taasisi ya Kitaifa ya Saratani katikati mwa mji wa Cairo.

Kulingana na taarifa ya wizara ya Ulinzi ya Misri gari moja lililokuwa linaendeshwa kinyume ya jinsi magari mengine yanavyokwenda liligongana na magari mengine matatu na kusababisha mripuko huo.

Kiongozi wa mashtaka ya umma wa Misri ameliambia shirika la habari la Reuters kuwa anachunguza chanzo cha tukio hilo. Hakujatolewa taarifa rasmi lakini inayoonyesha kwamba tukio hilo lilikuwa ni shambulizi.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad