Msanii wa Bobu Wine Atekwa na Kuuawa Kikatili



MWANAMUZIKI wa nchini Uganda, Ziggy Wine,  ambaye alikuwa chini ya usimamizi wa ‘Lebo’  ya mwanamuziki/mwanasiasa  Bobi Wine,  amefariki dunia usiku wa jmapili, Agosti 4, 2019.

Ziggy ambaye jina lake halisi ni Michael Kalinda,  amefariki baada ya kutekwa Julai 21,  mwaka huu, na kupigwa vibaya alipokuwa  njiani akielekea studio za Firebase Crew.  Inaelezwa kuwa baada ya watekaji kukamilisha unyama huo, walimtupa pembezoni mwa hospitali ya Mulago iliyopo jijini Kampala ambapo alikutwa akiwa amejeruhiwa vibaya huku jicho lake la kushoto likiwa limetobolewa, vidole vyake vya mkononi vikiwa vimekatwa.

Bobi Wine, Mbunge wa Kyadondo Mashariki  ambaye pia alikuwa akimsimamia Ziggy kimuziki,  tayari ameshazungumzia suala hilo, kupitia ukurasa wake wa Twitter ambapo ameandika:

“Ziggy alipatikana akiwa amejeruhiwa vibaya kwa kupigwa na kuteswa, jicho lake moja la kushoto likiwa limetolewa na vidole vyake viwili vikiwa vimekatwa, na zaidi ya hapo wamemuibia kila kitu alichokuwa nacho na kisha kumtupa pembeni ya hospitali ya Mulago”.

Vyanzo vya habari nchini Uganda vimeliambia gazeti la Daily Monitor  la nchini humo kuwa baada ya kutekwa na kujeruhiwa vibaya, Ziggy alilazwa katika Hospitali ya Mulago kwa zaidi ya wiki moja katika kitengo cha wagonjwa mahututi lakini hakupatiwa matibabu yoyote yanayostahili kwa makusudi, kitendo kilichofanya familia yake kulalamikia uongozi wa hospitali hiyo.

Ripoti kutoka hospitali hiyo inaeleza kuwa, Ziggy amefariki baada ya kujeruhiwa vibaya sehemu ya ubongo wake, na kuwa uchunguzi wa CT Scan ulibaini kuwa kuna damu nyingi ilivujia ndani ya ubongo.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad