Msemaji wa Serikali: Tumepokea kwa Masikitiko Taarifa ya Vifo vya Watu Vilivyotokana na ajali ya roli la mafuta Huko Morogoro

Msemaji Mkuu wa Serikali, Dkt. Hassani Abbasi amesema wamepokea kwa masikito taarifa kuhusu ajali ya roli la mafuta ililotokea Morogoro.

Dkt. Abbasi ameeleza kuwa Mkuu wa Mkoa na timu ya uokoaji wanaendelea kukabiliana na hali katika eneo la tukio.

"Tumepokea kwa masikitiko taarifa kuhusu ajali ya lori la mafuta,  Morogoro, iliyosababisha moto na kuunguza watu kadhaa. Mkuu wa Mkoa na timu za uokoaji wanaendelea kukabiliana na  hali katika eneo la tukio. Taarifa kamili kuhusu idadi ya vifo na majeruhi itatolewa badae," ameandika Dkt. Abbasi kwenye ukurasa wa Twitter.


Ameongeza kwa kusema kuwa "Tunaendelea kutoa wito kwa wananchi kukaa mbali na eneo la ajali hasa yanapohusika magari au vyombo vingine vya usafiri vilivyobeba vitu vinavyoweza kuripuka kama mafuta
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad