Mtwara: Amuua mkewe kisa 'kuchepuka',na yeye auawa

Kamishina Msaidizi wa Polisi Mkoa wa Mtwara Blasius Chatanda, amethibitisha kutokea kwa mauaji ya mwanaume mmoja aliyejulikana kwa jina la Juma Lugomba, Mkazi wa Kijiji cha Chiwata Wilaya ya Masasi, aliyeuawa na wananchi mara baada ya yeye kumcharanga kwa mapanga mke wake


na kisha kutokomea porini.

Kamishina Chatanda ameeleza sababu iliyopelekea mwanaume huyo kumuua mkewe,  kabla ya yeye kuuawa na wananchi ni alikuwa akimtuhumu mkewe huyo kuwa anamahusiano na wanaume wengine na ndipo alipojichukulia sheria mkononi .

"Baada ya kufanya mauaji hayo alikimbia lakini kwa vile taarifa zilikuwa zimeenea sana, wananchi walianza kumtafuta kimyakimya kwa sababu walikuwa wanajua anakofanyia shughuli zake za kuchoma mkaa, walimkuta huko wakamkamata na kumkatakata mapanga na yeye kisha kumchoma moto'' amesema Kamishina Chatanda.

Jeshi la Polisi linaendelea na uchunguzi ili kuwabaini wale wote waliohusika na mauaji ya mwanaume huyo, na kuwataka wananchi waache kujichukulia sheria mkononi.



Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad