Kinara wa chama cha upinzani cha Chadema, Tundu Lissu ametangaza kwamba amehitimisha matumizi ya dawa aliaonza kutumia Septemba 7, 2017.
Lissu amekuwa akitumia dawa na kupokea matibabu nchini Ubelgiji baada ya kushambuliwa na watu wasiojulikana ambao walimmiminia risasi zaidi ya 30 katika makazi yake Area D, Dodoma.
Kulingana na taarifa ya Mwananchi, Lissu aliwatumia marafiki zake ujumbe mnamo Jumatano Julai 31, 2019 akiwaarifu kwamba alikuwa amekamilisha matumizi ya dawa alizoanza kuzitumia tangu shambulio hilo na kwamba madaktari walimuhakikishiaafya yake iko salama.
"Kwa maelekezo ya daktari wangu jana (Jumanne) ilikuwa siku yangu ya mwisho ya mimi kuzitumia dawa nilizokuwa nikizitumia tangu nishambuliwe," alisema Tundu Lissu.
Kiongozi huyo aliongeza kwamba, licha ya hali yake ya afya kuimarika atasalia chini ya ulinzi wa madaktari hadi Agosti, 20 2019 ambapo atafanyiwa vipimo vya mwisho na kupata ushauri wa timu ya madaktari wake kabla ya kurejea nchini Tanzania.
Makaa hana, Hizo cheche feki atazitowa wapi.
ReplyDeleteHuyu bado madawa yana mzingua.
Hapa akirudi tunamgoja anayakujibu.
Huwezi kwenda kwenye vyombo vya uzushi na kutuharibia Taswira yetu na watu wake.
Mh Makonda alitoa waraka mzuri juu ya hawa genge la WaHaine/