Mwanaume Mmoja Afungwa maisha kwa Kumbaka Mzee wa miaka 74


Mwanamume mmoja raia wa Kenyan amehukumiwa kifungo cha maisha jela nchini Marekani kwa kumnyanyasa kingono ajuza wa miaka 74. limesema Shirika la habari la Dallas News.

Hatua hiyo inakuja miezi kadhaa baada ya mwanamume mwingine raia wa Kenya kushtakiwa kwa kuwaua wanawake wazee 11 mjini Texas.

Anthony Mamboleo Nyakeo anayesemekana kutekeleza kosa hilo mwezi Januari mwaka 2018 alipatikana na hatia ya kumbaka ajuza huyo wa wa miaka 74 aliyekuwa mgonjwa.


"Muuguzi aliyekuwa akimhudumia ajuza huyo alimpata anatokwa na damu katika sehemu zake za siri. Uchunguzi ulionesha muathiriwa amekuwa akidhulumiwa kingono mara kwa mara, huku uchunguzi wa chembembe za vinasaba uliofanyiwa wahudumu wote ukilingana na wa Nyakeo," mwendesha mashtaka aliiambia shirikala la habari la Dallas.

Nyakeo, alikuwa akifanya kazi kama muuguzi katika kituo cha afya cha Woodridge ambacho pia kinatoa huduma ya kuwarekekebisha watu tabia mjini Grapevine.

Ajuza huyo aliyekuwa na ugua ugonjwa wa Elzhema( unaosababisha kupoteza kumbukumbu) alifariki baadae mwaka huo.

Wakati wa kusikizwa kwa kesi hiyo, Mahakama ilifahamishwa kuwa Nyakeo alifanya kitendo hicho wakati muathiriwa wake hakuwa na uwezo wa kukubali au kukataa kutokana na hali yake kiakili.

"Hakuwa na uwezo wa kuzungumza, kujilisha walakujipeleka msalani na alikuwa akivishwaa diaper na wauguzi," Jordan Rolfe, mmoja wa waendesha mashataka aliiambia mahakama.

Bw. Nyakeo alikanusha mashtaka hayo akidai kwamba kuna mtu alitumia DNA kutoka kwa mpira wa kondomu uliotumika na kumwekea mama huyo.

"Nilimuogesha tu na kumpelea katika eneo la kula, "alisema Nyakeo.

Mfanyikazi Mwenzake aliyeotoa ushahidi dhidi yake alisema alipoonahali ya mwathiriwa moja kwa moja alishuku huenda amenyanyaswa kingono.

"Hiki si kitendo kianachofanywa kila siku hususan na wanawake wazee walio katika umri huo, kwa ufahamu wangu,"alisema.

Waendesha mashataka waliandika katika nyaraka za mahakama kuwa Nyakeo aliwahi kuwanyanayasa kimapenzi wafanyikazi wenzake na kwamba alijaribu kutoroka Texas wakati wa uchunguzi

"Alimwambia rafiki na mfanyikazi mwenzake wa zamani kudanganya kwa niaba yake wakati wa kutoa ushahidi " walinukuliwa katika nyaraka hizo.

Katika hoja ya kukamilisha kesi hiyo mwendesha mashtaka Jordan Rolfe aliwaambia majaji kuwa Nyakeo danastahili kufungwa kwa kufanya kitendo hicho cha kiajabu.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad