Mwandishi Kabendera amepooza “hawezi kupumua wala kutembea”

Mwandishi wa Habari za Kiuchunguzi, Erick Kabendera anayekabiliwa na kesi ya Uhujumu Uchumi katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu anadaiwa hawezi kupumua vizuri na kutembea kwa sababu amepooza mguu.

Kutokana na hatua hiyo, Upande wa utetezi kupitia Wakili Jebra Kambole umeiomba Mahakama itoe amri ili mshitakiwa huyo akatibiwe.

Hayo yameelezwa mbele ya Hakimu Mkazi, Janeth Mtega baada ya Wakili Mwandamizi wa Wakili Serikali, Wankyo Saimon kueleza upelelezi wa kesi hiyo haujakamilika, hivyo wanaomba ahirisho.

Baada ya kueleza hayo, Wakili Kambole amedai usiku wa kuamkia Agosti 2,2019 mteja wake akiwa gerezani alianza kuumwa na hadi leo ana shida ya kupumua.

“Nilienda kumuona nikakuta amepooza mguu na kushindwa kutembea kwa siku mbili pamoja na kuishiwa nguvu sisi kama mawakili na ndugu hatujui nini anachoumwa” amedai Wakili Kambole

“Kwa kuwa mteja wetu hajapata vipimo ambavyo vinastahili tunaomba Mahakama ielekeze Jeshi la magereza mteja wetu akapimwe katika hospitali yoyote ya serikali ikiwemo Muhumbili penye vipimo vya uhakika”

Wakili Wankyo amedai swala la ugonjwa hakuna mtu anayeweza kupingana nalo lakini huwezi kulielekeza jeshi la magereza kwenda kumpima katika hospitali fulani.

“Mahakama yako haiwezi kuamuru kupelekwa hospitali fulani kwa kuwa hajawahi kuwasilisha maombi akakataliwa lakini sheria inasema makosa ya uhujumu uchumi yanasikilizwa na Mahakama kuu hivyo Mahakama hii haina uwezo wa kutoa uwamuzi wowote” alieleza Wakili Wankyo

Hata hivyo, Hakimu Mtega baada ya kusikiliza hoja za pande zote aliahirisha kesi hadi Septemba 12, 2019 itakapotajwa.

Kabendera alifikishwa Mahakamani kwa mara ya kwanza, Agosti 5, 2019 akikabiliwa na mshtaka matatu, ambayo ni kuongoza genge la Uhalifu, kukwepa kodi na kutakatisha zaidi ya Sh. 173.2Milioni.

Pia anadaiwa katika siku tofauti tofauti kati ya Januari 2015 na Julai 2019 katika maeneo tofauti jijini Dar es, Salaam, mshtakiwa Kabendera alitoa msaada katika genge la uhalifu kwa nia ya kujipatia faida.
Tags

Post a Comment

1 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Sukri inamsumua siku nyingi.

    Hapo hapo aendelee na vidonge na mazoeezi. Ulimi haauja pooza .

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad