Mwenyekiti wa Schalke 04, Ajiuzulu Kufuatia Matamshi ya Kibaguzi Dhidi ya Afrika

Mwenyekiti wa Schalke 04, Ajiuzulu Kufuatia Matamshi ya Kibaguzi Dhidi ya Afrika
Mwenyekiti wa klabu ya soka ya Schalke 04 ya Ujerumani, Clemens Tönnies amelazimika kujiuzulu nafasi hiyo kwa muda kufuatia matamshi yake ya wiki iliyopita yaliyo ilenga bara la Afrika ambayo yamekosolewa kuwa ya kibaguzi.

Akizungumza kwenye mkutano mjini Paderborn baada ya kukutana na wageni 1,600 wiki iliyopita, Tönnies mwenye umri wa miaka 63, anaripotiwa kukosoa kuongezwa kwa kodi kwa ajili ya kupambana na mabadiliko ya tabia nchi na kupendekeza kuwa ni heri kujenga viwanda 20 vya kuzalisha umeme kila mwaka barani Afrika ili Waafrika waache kukata miti na pia waache kutafuta watoto wakati giza linapoingia.

Hata hivyo ameomba radhi kwa matamshi yake aliyotoa kwa niaba ya klabu hiyo akiamini kuwa ni ya kibaguzi. Na baada ya matamshi yake kulaaniwa sana na mashabiki wa klabu ya Schalke, bodi ya klabu hiyo imetoa taarifa na kusema kwamba mwenyekiti huyo amejiuzulu wadhfa wake japo kwa miezi mitatu tu kwa kuwa imempata na hatia ya kwenda kinyume na sera zinazopinga ubaguzi za klabu hiyo.

Shirikisho la Soka la Ujerumani, DFB, limesema kuwa ni jambo la kushtusha na kusikitisha kuona kwamba mtu mwenye nafasi na uzoefu mkubwa kama Tönnies anatoa matamshi mabaya kama hayo kuhusu watu wa bara zima.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad