Naibu Spika Dkt. Tulia Ackson atangaza kugombea ubunge 2020.


Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Tulia Ackson ameweka wazi kuwa mwaka 2020 atagombea ubunge kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi (CCM).


Dkt. Tulia ameweka wazi mipango hiyo leo Agosti 19, 2019 kwenye mahojiano yake na kituo cha East Africa Radio, Ambapo amesema anaamini yeye ni mchapakazi na ndio maana amekuwa akiteuliwa katika nyadhifa mbalimbali.

“Kuhusu watu wanaosema kuwa mimi mafanikio yangu yamekuwa ya haraka sana, hilo kuna watu wa kulizungumzia nataka kuamini watu ambao wamekuwa wakiniteua itakuwa wameona kazi niliyokuwa nikiifanya.“ameongea Dkt. Tulia na kuweka wazi malengo yake ya kugombea Ubunge mwakani.

“Mwenyezi Mungu akitupa Uhai 2020 nitagombea, ila nitagombea wapi? naomba watulie kwa sababu chama chetu kina utaratibu wake ila nashukuru ninavyoonekana nina uwezo wa kugombea maeneo mengi.“amesema Dkt. Tulia.

Tangu mwaka jana kumekuwa na tetesi kuwa Dkt. Tulia atagombea jimbo la Mbeya Mjini kwa tiketi ya CCM kwenye uchaguzi Mkuu mwakani. Jimbo hilo kwa sasa lipo chini ya CHADEMA na linaongozwa na Mhe. Sugu.

Post a Comment

4 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. HONGERA kwwa Nia yako mama Tulia.
    Tuna mwambia mwa hip hop arudie kutafuta Gita lake na nyadhifa mpya na atulipe tuli.

    MAMA Tulia anakuja na mchaka mchaka. Alimselema Alijaaah.

    Mbeya yetu tunaichukua ili kuiletea MAENDELEO stahiki na Si mikiki na upingaji WA KILA kitu.

    Mbeya Oyeeeee..!! Dkt Bashir Alisha peleka Salam na MAMA TULIA ANAKUJAAAAAAA

    ReplyDelete
  2. Mama Ushindi wako.
    Utakuwa NI WA Kishindo tuuuuu

    ReplyDelete
  3. Kuna Tetesi hivi punde Sugu ampelekwa Hospitali baada ya mshinikizo wa Damu uliokuwa si wa kawaida alipokuwa akisoma na Kuperuzi Mitandao mchana huu...!!

    plesha imeshamuanza kwa habali hii....!!

    ReplyDelete
  4. Mbilinyi, Pole Aise....!!!

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad