Ndege ya Urusi yalazimika kutua kwa dharura baada ya kugongana kundi la ndege


Ndege ya abiria ya Urusi imelazimika kutua kwa dharura kwenye shamba la mahindi karibu na jiji la Moscow baada ya kugonga kundi la ndege.

Watu ishirini na watatu wamejeruhiwa katika tukio hilo, ambalo limesababisha ndege kutua huku injini yake ikiwa imezima na gia yake kutua ikirudi nyuma, wamesema maafisa wa afya.

Ndege hiyo Ural Airlines Airbus 321 ilikuwa ikisafiri kuelekea katika eneo la Simferopol Crimea ilipogonga kundi la ndege muda mfupi baada ya kuondoka uwanjani , hali iliyovuruga utendaji wa injini yake.


Vyombo vya habari vya taifa la Urusi vimetaja kutua kwa ndege hiyo kama "muujiza wa eneo la Ramensk".

Maafisa wa ndege hiyo wamesema ndege imeharibika sana na haiwezi kupaa tena. Uchunguzi rasmi juu ya ajali hiyo unaendelea.


Ndege ya abiria yatua kwa ghafla baada ya kugongana na kundi la ndege
Ndege hiyo ilikwa na abiria 233 na wahudumu ndani yake wakati ndege waliporipotiwa kuingia ndani ya injini na rubani wake akaamua kutua mara moja.

Abiria mmoja ambaye hakutajwa jina lake ameiambia televisheni ya taifa kuwa ndege ilianza kuyumba kwa hali ilisiyo ya kawaida baada ya kuondoka uwanjani.

"Sekunde tano baadae, taa za upande wa kulia za ndege zikaanza kuwaka na kuzima na kulikuwa na harufu ya kuungua. halafu tukatua na kila mtu akatimua mbio kwenda mbali ," alisema.


Shirika la usafiri wa ndege la Rosaviatsia limesema kuwa ndege hiyo ilitua katika sahamba la mahindi yapata kilomita moja (maili 0.62 ) kutoka kwenye njia yake kwenye uwanja wa kimataifa Zhukovsky , huku injini yake ikiwa imezima na breki zake za kutua zikiwa zimerudi nyuma.

Wasafiri walitolewa kutoka kwenye ndege, huku baadhi wakipelekwa hospitalini kwa matibabu na wengine wakiongozwa kuelekea kwenye uwanja wa ndege.

Wizara ya afya imesema kuwa watoto watano walikuwa miongoni mwa wasafiri waliolazwa kufuatia ajali hiyo.. Wale waliojeruhiwa katika mkasa huo walichukuliwa kama watu wenye "hali mbaya na hali ya kawaida ",imesema.

Mkurugenzi Mkuu wa kampuni ya ndege ya Ural Airlines Kirill Skuratov amewaambia waandishi wa habari kuwa wasafiri waliotaka kuendelea na safari yao watawekwa kwenye ndege mbadala baada ya kufanyiwa uchunguzi wa kimatibabu.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad