Nikiondoka Watakaokuja Watayamaliza Kweli? - Rais Magufuli



Rais wa Tanzania, Dkt. John Magufuli amesema hana uhakika iwapo viongozi watakaokuja baadae wataweza kuingoza nchi na kuiletea maendeleo kama ilivyo sasa kutokana na kazi hiyo kuwa ngumu.

“Mara nyingi tumeambiwa kuwa Tanzania ni masikini, ninaomba neno hilo tulifute kwani nchi yetu ni tajiri lakini tulitaka kuaminishwa na watu waliotaka kututumia, kuna miradi imetumia matrilioni ya fedha saa nyingine ninajiuliza kweli hili limewezekana, tumeweza maana yake kila palipo na nia Mungu yupo pamoja na sisi,” amesema.

“Siwezi nikasimama mbele za watu nikasema haya ni kwasababu yangu kwani mimi ni dereva tu lakini pia huwa ninajiuliza ikitokea siku Mungu akanichukua hao watakaokuja watayamaliza kweli kwasababu panahitaji moyo, unafanya hivi huku unatukanwa lakini inabidi ufanye kwaajili ya Watanzania, inahitaji kujitoa sadaka ya kweli,” amesema.

Rais Magufuli ametoa kauli hiyo leo, alipokuwa akizungumza katika hafla ya ufunguzi wa jengo la tatu la abiria katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA), jijini Dar es Salaam ambapo amesema kuwa Tanzania sasa imekuwa mfano wa kuigwa na nchi nyingine.

Post a Comment

2 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Tunakuombea Mwenyezi mungu akulinde
    na Akupe Afya Njema na Umuri mrefu
    kwa Baraka za Mwezi mtukufu wa Dhul Hijja. na Hata ukimaliza muda wako huko2028 .Wewe utaendelea kuwa Mshauri mkuu wa atakae kuwa Madarakaani wakatihuo. Nakuomba ututayarishie Kwa maono yangu kijana anaejifunza na kujituma na muadilifu na ni mchapa kazi kweli kweli katika ufatiliaji waangu on Perfomance Jaffo ni mmoja wapo na inshaallah mngu ampe afya ni msikivu na mfatiliaji kama ulivyo wewe
    Jemedari wetu.

    Mlungu akutaze mwaha.
    Mpelaje milimo mzelelo.

    Magu wetu unaandika Historia kwa wnoo wa Dhahabu inshallah Allah ataulindana kukupa Subira. Na mwenyezi mungu atamuafu Mama ainuke Salama Salmin.

    ReplyDelete
  2. Tunakuombea Mwenyezi mungu akulinde
    na Akupe Afya Njema na Umuri mrefu
    kwa Baraka za Mwezi mtukufu wa Dhul Hijja. na Hata ukimaliza muda wako huko2028 .Wewe utaendelea kuwa Mshauri mkuu wa atakae kuwa Madarakaani wakatihuo. Nakuomba ututayarishie Kwa maono yangu kijana anaejifunza kutoka kwako na kujituma na muadilifu na ni mchapa kazi kweli kweli katika ufatiliaji waangu on Perfomance Jaffo ni mmoja wapo na inshaallah mngu ampe afya ni msikivu na mfatiliaji kama ulivyo wewe
    Jemedari wetu.

    Mlungu akutaze mwaha.
    Mpelaje milimo mzelelo.

    Magu wetu unaandika Historia kwa wnoo wa Dhahabu inshallah Allah ataulindana kukupa Subira. Na mwenyezi mungu atamuafu Mama ainuke Salama Salmin.

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad