Haji Omar Kheri ameeleza hayo wakati akizungumza na watendaji na viongozi wa chama na
serikali katika mkutano wa majumuisho wa ziara aliyoifanya katika Mkoa wa Mjini Magharibi uliofanyika katika ukumbi wa sheikh Idrisa Abdul Wakil kikwajuni Mjini Unguja.
Amesema wizara ya Tawala za Mikoa ipo tayari kushirikiana na taasisi nyengine katika
kuharakisha kasi ya maendeleo na kukuza uchumi wan a kuimarisha ustawi wa jamii.
“Sisi kama wasimahizi wa wizara hii ya Tawala za Mikoa kwa maana ya Mikoa Wilaya na
Maspaa tupo tayari tangu jana kushirikiana na kufanya kazi kwa pamoja Katika kuwahumia wananchi maana sisi ndio jukumu letu la msingi”alisema waziri Kheir.
Aidha Mheshimiwa Haji amesema Serikali ikuja na dhana ya utalii kwa wote hiyo wizara yake itashirikiana na wizara husika ili kuona sekta ya utalii inaendelea kuimarika na kuziondoa baadhi ya changamoto zinazoikabili sekta hiyo kwa maslahi ya wananchi na taifa kwa ujumla.
“Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imekuja na mpango huu wa utalii kwa wote kwa maana ya
ushirikishwaji wa taasisi mbali mbali na sisi tunashiriki kikamilifu kwa maslahi ya wananchi wetu maana sekta ya utali inamchango mkubwa kwa uchumi wa nchi”alisema waziri Haji.
Katika hatua nyengine Waziri Haji amewataka viongozi wa serikali ya Mkoa,Wilaya na Manispaa
za Mkoa Mjini Magharibi kuhakikisha inazifanyia kazi maigizo na maelekezo yote yaliyotolewa wakati wa ziara hiyo na kuyapatia ufumbuzi kwa wakati.
“Napenda kusisitiza yale niliyoyaagiza na kuelekeza yafanyiwe kazi kwa haraka kama
tulivyoelekezana isingojewe mpaka nikafanya ziara tena maana ikifika tarehe mosi mwezi ujao nitaenda kuangalia kijangwani sasa harakisheni”alisema Mheshimiwa Haji.
Katika hatua nyengine Mheshimiwa Haji ameugiza uongozi wa baraza la manispaa ya Mjini
kuondosha ukuta uliojengwa katika bustani ya botanic iliyopo kilimani ili kuliacha eneo hilo kutumika kwa matumizi yaliyokusudiwa.
“Niliagiza ule ukuta uliojengwa pale katika bustani ya Botanic Kilimani uondolewe lakini
muda umepita haujaondolewa na badala yake kumekatwa viwanja.
Hata hivyonawapongeza wale walioenda kuzuwia ujenzi na sasa nasema tena ukuta ukaondoshwe
tufuate utaratibu wa kufuta kibali kama tumetoa, eneo lile lina mipango mizuri ya kuliendeleza kwa kutengeneza bustani ya kisasa wenzetu wa Ujerumani watatusaidia”, alisema Mheshimiwa Haji.
Mapema akizungumza katika Mkutano huo, Mkuu wa Mkoa Mjini Magharibi Ayoub Mohammed
Mahmoud amesema serikali ya mkoa huo utayafanyia kazi maagizo na maelekezo yote yaliyotolewa wakati wa ziara na kuharakisha inakoleza kasi ya maendeleo katika Mkoa huo.