Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) wilaya ya Ilala inamshikilia Ofisa Kodi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Elias Yunus (38) kwa tuhuma za kuomba rushwa ya shilingi milioni 50 kwa ahadi ya kumsaidia mfanyabiashara aliyetaka kukwepa kodi.
Akizungumza na waandishi wa habari leo Ijumaa, Agosti 2, Kaimu Mkuu wa Takukuru wilaya ya Ilala, Enock Ngailo amesema mtuhumiwa huyo alikamatwa baada ya kuomba rushwa kwa mfanyabiashara raia wa Uturuki (jina limehifadhiwa), ambaye ni Mkurugenzi wa Kampuni ya Heavy Equipments Company Ltd.
Ngailo amesema ofisa huyo alitengeneza mazingira ya rushwa baada ya mfanyabiashara kutoa taarifa za uongo katika usajili wa mtambo aliouingiza kutoka nje ya nchi kwa lengo la kukwepa kodi kinyume na kifungu cha Sheria ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Na. 11 ya mwaka 2007, mtuhumiwa aliomba rushwa ya Sh milioni 50 na tayari amepokea Dola za Marekani 1,000.
“Uchunguzi wa Takukuru umebaini mtuhumiwa aliomba rushwa hiyo na baada ya majadiliano alipunguza kiasi hicho na kufikia Sh milioni 35 kwa masharti ya kupewa fedha hizo zikiwa katika Dola za Marekani (Dola 17,000)'', amesema Ngailo.
Kweli huyo Hamnazo..!!
ReplyDeleteUnaomba Rushwa katika awamy ya /magufuli…!!!
Sasa Utanyea Debe na ukija Toka umechoka na kokote Ajira huwezi kupata itabidi urudi kijijini ukalime Nyanya na Mchicha.
Watu wanatafuta Kodi.. Wewe unataka kusamehe na kujinufaisha wakati huo huo.
Punguani wewe nani atajenga Hospitali na kukulipa wewe mshahara wako..???
Umeshindwa kusoma Alama za Nyakati..!!!