Ofisi Zapakwa Kinyesi cha Binadamu

Katika kipindi cha miezi miwili iliyopita, zaidi ya ofisi 10 za chama cha upinzani nchini Burundi - (CNL) zimekuwa zikiharibiwa ima kwa kuchomwa moto au kupakwa kinyesi cha binadamu.

Muakilishi wa chama hicho ameiambia BBC kuwa vitendo hivyo ni juhudi za kuzuwia demokrasia na kuutisha upinzani, kabla ya uchaguzi wa urais wa mwaka 2020.


Therence Manirambona, msemaji wa CNL ameieleza BBC namna ofisi zao za Bubanza, Cibitoke, Ngozi, Rumonge na Bujumbura zilivyoporwa, kuteketezwa kwa moto ima kupakwa kinyesi cha binadamu.

''Ofisi ya CNL Gatete iliyopo wilayani Rumonge, magharibi mwa Burundi, ndio ofisi ya hivi karibuni kushambuliwa kwa vitendo hivyo ambapo ofisi hiyo ilishambuliwa Jumanne Julai, kwa moto. ulioteketeza ofisi'', amesema Therence Manirambona.

Image caption
Ofisi ya CNL
Mapema mwezi huu, Wachunguzi wa Tume ya haki za binadamu ya Umoja wa Mataifa kuihusu Burundi walitoa ripoti juu ya 'ukiukaji mkubwa ' wa haki za kibinadamu nchini Burundi, unaoulenga upinzani.

Mwanasiasa wa upinzani anayedaiwa kupanga kumuua Rais Pierre Nkurunziza
Muwakilishi wa Burundi katika tume ya Umoja wa Mataifa mjini Geneva aliitaja ripoti hiyo kama 'waraka wa uongo'.

Bwana Manirambona amesema kwamba "kuzipaka ofisi zao kwa kinyesi cha binadamu ni kitendo cha chuki isiyo ya kufikirika ".

Image caption
Baadhi wa wanachama wa chama cha CNL wakiwa mbele ya ofisi yao iliyoharibiwa
Bwana Manirambona ameelezea kusikitishwa kwake na kwamba katika nchi yenye taasisi nyingi za usalama na upelelezi , hakuna mtu hata mmoja aliyekamatwa au hata kuhojiwa kuhusiana na vitendo hivyo viovu vinavyoendelea kwenye ofisi zao.

"Kwa hili , tunadhani kwamba hivi ni vitendo vya uchochezi wa kisiasa dhidi yetu, kwasababu katika ngazi za mwanzo baadhi ya watu wanasema kwamba CNL isingepaswa kuwa na ofisi katika maeneo yao " amesema Manirambona.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad