Spika Ndugai Afungua Mkutano Wa Wabunge Kutoka Bara La Asia Na Afrika Unaohusu Masuala Ya Idadi Ya Watu Na Maendeleo Jijini Dar Es Salaam
0
August 06, 2019
Spika wa Bunge, Job Ndugai amesema Bunge litaendelea kuishauri Serikali kuhusu mambo mbalimbali ya idadi ya watu na maendeleo ili kuliwezesha Taifa kufikia dira yake ya maendeleo ifikapo 2025 na malengo endelevu ya maendeleo (SDG).
Aliyasema hayo jana jijini Dar es Salaam akifungua mkutano wa wabunge wa Afrika na Asia unaolenga kubadilishana uzoefu katika masuala ya ongezeko la idadi ya watu na maendeleo.
Ndugai alisema Dira ya Taifa ya Maendeleo ya 2025 ilianzishwa baada ya mkutano wa kimataifa wa idadi ya watu na maendeleo (ICPD). Hivyo, kama mshiriki, Tanzania ilinufaika na mkutano huo na kutengeneza dira yake ya maendeleo mwaka 2000.
Kuhusu suala la ongezeko la idadi ya watu, Ndugai alisema ongezeko katika ngazi ya familia linatakiwa kuendana na kiwango cha uchumi kwa familia husika ili watoto waweze kupata huduma muhimu za kijamii.
Ndugai alisema lazima nchi za Afrika zifikirie namna ya kugeuza idadi ya watu kama fursa ya kujiletea maendeleo, lakini kudhibiti ongezeko la watu ili kila mtu ngazi ya familia hadi Taifa aweze kupata huduma muhimu.
Tags