Omar al-Bashir afikishwa mahakamani, yadaiwa kukutwa fedha katika magunia ya nafaka nyumbani kwake


Afisa wa uchunguzi ameiambia mahakama nchini Sudan kwamba rais wa zamani Omar al-Bashir amekiri kupokea mamilioni ya dola kutoka Saudi Arabia.



Bashir

Bashir alifika mbele ya mahakama leo Jumatatu kukabiliwa na mashtaka ya ufisadi, ambayo mawakili wake wanasema hayana msingi.

Alitimuliwa madarakani Aprili baada ya maandamano ya miezi kadhaa, yaliofikisha kikomo utawala wake wa takriban miaka 30.

Mnamo Juni, waendesha mashtaka wamesema kiwango kikubwa che fedha za kigeni zilizohodhiwa ziligunduliwa katika magunia ya nafaka nyumbani kwake.

Siku ya Jumapili, wanaharakati wa kutetea demokrasia na viongozi wa jeshi nchini humo waliomtimua madarakani Bashir, walisaini makubaliano yanayotoa fursa kufanyika uchaguzi mkuu nchini.

Kiongozi huyo wa zamani, aliyefika mahakamani na kusimama kizimbani alikuwa amevaa nguo nyeupe na kilemba. Hakujibu tuhuma zinazomkabili, Shirika la habari la Reuters linaripoti.

Kumekuwa na maafisa wengi wa usalama walioshika doria nje ya mahakama katika mji mkuu Khartoum, wakati Bashir alipowasili.Sudan's ex-President Omar al-Bashir leaves the office of prosecutor in Khartoum, Sudan - Sunday 16 June 2019

Bashir alionekana kwa mara ya kwanza hadharani mnamo Juni mjini Khartoum

Anakabiliwa na mashtaka gani ya ufisadi?

Kwa mujibu wa shirika la habari la BBC, Kiongozi huyo wa zamani anakabiliwa na mashtaka yanayohusiana na “kumiliki fedha za kigeni, ufisadi, na kupokea zawadi kinyume cha sheria”.

Mnamo April, kiongozi wa jeshi Sudan Abdel Fattah al-Burhan alisema zaidi ya milioni $113 ya fedha katika sarafu ya pauni ya Sudan na sarafu za kigeni ziligunduliwa numbani kwake Bashir.

Mawakili wanaomtetea Bashir wanapinga mashtaka hayo.

Kiongozi huyo aliyetimuliwa alitarajiwa mahakamani mnamo Julai – lakini kesi iliahirishwa kutokana na sababu za usalama.

Bashir anakabiliwa na mashtaka gani mengine Sudan?

Mnamo Mei, nwendesha mashtaka nchini Sudan alimshtaki Bashir kwa uchochezi na kuhusika katika mauaji ya waandamanaji.

Mashtaka hayo yanatokana na uchunguzi wa kifo cha daktari aliyeuawa wakati wa maandamano yaliochangia kutimuliwa kwa Bashir madarakani mnamo Aprili.Demonstrators in Sudan. Photo: July 2019Kumeshuhudiwa maandamano ya miezi kadhaa Sudan

Shahidi mmoja ameieleza BBC kwamba daktari huyo aliyekuwa akiwatibu majeruhi alitoka nje ya jengo akiinua mikono juu, na kuarifu polisi kwamba yeye ni daktari, na papo hapo akapigwa bunduki.

Kesi ya Omar el Bashir ina uzito gani?

Kesi ya Bashir inaonekana kama mtihani wa iwapo utawala mpya unaweza kukabiliana na uhalifu unaotuhumiwa kutekelezwa na utawala uliokuwepo.

Siku ya Jumamosi, baraza la utawala wa kijeshi nchini ulioingia madarakani baada ya kuondoka kwa Bashir, lilisaini makubaliano muhimu ya ugavi wa mamlaka na muungano wa kiraia wa upinzani.

Makubaliano hayo yanatoa fursa ya kuidhinishwa baraza jipya la utawala linalowajumuisha raia na majenerali wa jeshi , na kutoa fursa ya kufanyika uchaguzi mkuu na hatimaye utawala wa kiraia.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad