Omar al-Bashir kuomba kuachiwa kwa dhamana katika kesi ya rushwa


Wakili wa rais wa zamani wa Sudan Omar al-Bashir amesema kuwa atawasilisha ombi la kutaka Bashir aachiliwe kwa dhamana wakati kesi yake ya mashitaka ya rushwa ikiendelea.

Ahmed Ibrahim amewaambia wanahabari nje ya mahakama kuwa wataiomba mahakama kumuwachia kwa dhamana kwa sababu hiyo ni kesi ya kawaida.

Bashir anashitakiwa kwa kumiliki kinyume cha sheria fedha za kigeni na kupokea zawadi katika njia isiyo rasmi. Wakati wa kusikilizwa kesi yake, jaji alitaka kupewa ombi la dhamana kupitia maandishi, akisema ofisi yake iko tayari kulipokea wakati wowote.

Afisa wa polisi aliiambia mahakama Jumatatu kuwa Bashir alikiri kupokea mamilioni ya dola kutoka kwa Saudi Arabia.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad