Orodha ya Waliochaguliwa Kujiunga na Kidato cha Tano, 2019 Awamu ya Pili

Jumla ya wanafunzi 1674 kati ya wanafunzi 1,861 waliokuwa wanasuburi chaguo la pili la kujiunga na kidato cha tano, wamepewa nafasi hiyo baada ya kuwa na sifa zinazotakiwa.

Hayo yalibainishwa jana na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Mhe. Selemani Jafo wakati  akiongea na waandishi  wa habari kuhusiana na uchaguzi wa wanafunzi katika chaguo la pili( Second Selection).

Amesema kuwa wanafunzi 187 wameshindwa kuchanguliwa kutokana na tahasusi (combination) zao kutokuwa na ulinganifu unaotakiwa.

Mhe. Jafo amesema kuwa kati ya wanafunzi 1,674 waliochaguliwa ni wanafunzi 1497 ambao wamepangiwa masomo ya sanaa na biashara wakati wanafunzi 178 watajiunga na masomo ya sayansi na hisabati.

Akifafanua zaidi amesema wanafunzi hao wanatakiwa kuanza kuripoti katika shule walizochaguliwa kuanzia Septemba 2 hadi 16 mwaka huu na kuwa watakaoshindwa kufanya hivyo watakuwa amepoteza nafasi hiyo.

“Pia nitoe wito kwa wanafunzi 187 ambao wameshindwa kuchaguliwa kwasababu ya tahasusi zao kutokuwiana (balance) waombe kusoma kwenye vyuo vya ufundi ambayo vinasimamiwa na Baraza la Vyuo vya Ufundi (NACTE).

Hivi karibuni Jafo alitangaza uchaguzi wa wanafunzi wa kijiunga na kidato cha tano awamu ya kwanza na kubainisha kuwa jumla ya wanafunzi 108,644 ambao ni sawa na asilimia 98.31, walichaguliwa kujiunga na kidato cha tano na vyuo vya ufundi ikiwa ni kati ya wanafunzi 110,505 wenye sifa.

Mhe. Jafo alisema kuwa kati ya wanafunzi hao, wanafunzi 69,356 ambapo wasichana ni 31,809 na wavulana 37,547 wamechaguliwa kujiunga na kidato cha tano ambao ni sawa na asilimia 62.76 ya wanafunzi 110,505 ya waliokuwa na sifa

Waliochaguliwa kujiunga kidato cha tano kuwa ni 35,703 waliochaguliwa tahasusi ya Sayansi na Hisabati, kati yao wasichana ni 14,876 na wavulana 20,827 huku wa tahasusi ya Sanaa na Biashara ni 33,653, wasichana wakiwa ni 16,934 na wavulana ni 16,719.

 Waliojiunga na shule za wanafunzi wenye ufaulu mzuri zaidi (vipaji maalum) ni 1,462 ambapo wasichana ni 646 na wavulana 816. “miongoni mwao wanafunzi 6 ni wenye mahitaji maalumu ambao wasichana ni watatu na wavulana watatu.

Alisema wanafunzi wenye mahitaji maalumu waliochanguliwa ni 157 ikiwa wasichana ni 74 na wavulana ni 86 wakati wanafunzi waliochanguliwa ambao waliosoma chini ya taasisi ya Elimu ya Watu Wazima ni 174 ikiwa ni wasichana 74 na wavulana 100.

Aidha Mhe. Jafo ametoa wito  kwa wanafunzi waliopangwa awamu ya pili kuripoti kuanzia tarehe 2 Septemba, 2019 na wanafunzi watakaoshindwa  hadi kufikia tarehe 16 Septemba, 2019 atakuwa amepoteza  nafasi yake

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad