Paul Pogba Afunguka Ishu ya Ubaguzi wa Rangi

Kiungo mshambuliaji wa Manchester United, Paul Pogba amefunguka kuwa sakata lake la kubaguliwa kisa rangi yake kumempa nguvu ya kuwa imara zaidi. Pogba amesema ubaguzi wa rangi kwake anaona ni ushamba na unapoteza muda kufanya mambo makubwa.

Ikumbukwe Pogba alishambuliwa kwenye mitandao ya jamii baada ya kushindwa kufunga penalti kwenye mchezo wa ligi kuu Uingereza (EPL) dhidi ya Wolves na kutoka sare ya 1-1.

Wakati huo huo, kocha wa Man U Ole Gunnar Solskjaer amesema sasa anamruhusu Paul Pogba kupiga penalti baada ya Marcus Rashford aliyekuwa akimwamini kukosa mkwaju wa penalti dhidi ya Crystal Palace kwenye ligi kuu Uingereza.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad