Kamishna wa Operesheni na Mafunzo wa Jeshi la Polisi, Liberatus Sabas amesema mabasi yanayotoka Dar kuelekea Mikoa ya Kagera, Kigoma, Katavi hayataruhusiwa kutembea saa 24 kutokana na sababu za kiusalama
-
Amesema mabasi yanayotoka Dar es Salaam kuelekea katika mikoa hiyo yatalazimika kulala Wilayani Kahama kisha kuendelea na safari
-
Ameongeza kuwa zuio hilo litahusu pia mabasi yanayotoka Dar kuelekea Wilaya mbalimbali za Tabora ambapo yatalazimika kusimama Tabora Mjini na baadaye kuendelea na safari Wilayani
-
Aidha, mabasi yanayotoka Kagera, Katavi, Kigoma kwenda Dar yataruhusiwa kutembea saa 24 kama kawaida kutokana na eneo la Morogoro na Dar kuwa salama wakati wote
-
Takribani mwezi mmoja uliopita, Waziri wa Mambo ya Ndani, Kangi Lugola alipiga marufuku Makamanda wa Polisi wa Mikoa kuzuia mabasi yanayosafiri kati ya Dar na Mikoa ya Kanda ya Ziwa kusafiri usiku kwa kisingizio cha kuhofia kuvamiwa na majambazi - #regrann