Jeshi la Polisi mkoa wa kipolisi Tarime na Rorya wamewaua watu watatu wanaosadikiwa kuwa majambazi wa vitendo vya uhalifu na unyang'anyi wa kutumia silaha za moto.
"Tarehe 05,08,2019 majira ya saa 08 usiku katika kitongoji cha Makerero kijiji cha Nyamwaga kata ya Nyamwaga mkoa wa kipolisi Tarime na Rorya Askari wa kikosi cha kupambana na uhalifu walifanikiwa kuwaua majambazi watatu wanaojihusisha na vitendo vya uhalifu wa unyang'anyi wa kutumia silaha pamoja na mauaji kamanda mkoa wa kipolisi Taraime na Rorya, Henry Mwaibambe," alisema.
Kamanda huyo aliongeza kusema kuwa kati yao moja ya majambazi hao alijulikana kwa jina la Emanuel Marwa Kenara 35 mkazi wa kijiji cha Nyamwigura huku majambazi wengine majina yao hayajatambuliwa ambao wanakadiriwa kuwa na miaka kati ya 30 hadi 45 na wote ni wanaume.
Mwaibambe aliongez kuwa mara baada ya Askari kumkamata Emanuel Kenara jambazi huyo tarehe 03,08,2019 alikuwa tayari kuwaonyesha askari polisi mahali alipoficha silaha anayoitumia kufanyia uhalifu.
Polisi na mhalifu huyo wakiwa wanaelekea katika eneo la tukio ambapo silaha hiyo imefichwa ndipo ghafla majambazi wenzake wawili walianza kuwashambulia askari polisi kwa risasi za moto ambapo polisi walijibu mapigo na kufanikiwa kuwapiga risasi majambazi hao aliongeza kusema Mwaibambe.
Mwaibambe aliongeza kuwa Emanueli Marwa Kenara naye alipata mwanya na kutaka kutoroka/kukimbia ndipo walipigwa risasi na polisi na kujeruhiwa sehemu mbalimbali za miili yao ambapo Askari waliwachukua kuwapeleka hospitali kwa matibabu kwa bahati mbaya wakafia njiani kabla hawajafika hospitali wakipelekwa kwa matibabu ili kuoka maisha yao.
Mwaibambe alifafanua mbele ya waandishi wa habari Ofisini kwake jana kuwa kwenye eneo la tukio yamepatikana maganda manne ya risasi ya AK-47 silaha iliyofutwa namba ikiwa na risasi Tano kwenye Magazine na simu mbili za mkononi pia miili ya marehemu hao imehifadhiwa katika hospitali ya wilaya inayomilikiwa na halmashauri ya Mji wa Tarime kwa uchunguzi wa Madakitari.
Kamanda huyo aliwataka wakazi wa Tarime na Rorya ili kuacha kujihusisha na vitendo vua kiuhalifu kwasababu mkono wa sheria ni mrefu na utawasaka na kuwakamata popote watakapokuwa