Poshy: Sitaki Mahari Kubwa Baadaye Isije Kutumika Kama Fimbo

MREMBO mwenye umbo matata Bongo, Jacqueline Obeid ‘Poshy Queen’ amesema pindi utakapofika wakati wa kuolewa, hataki mahari kubwa ili baadaye isije kutumika kama fimbo ya kumchapia.

Akizungumza na Amani, Poshy alisema watu wengi wanafikiri msichana ukitolewa mahari kubwa ni sifa kumbe ni kujitengenezea wakati mgumu mbele ya safari kwa mwanaume kukutumikisha akiamini amekununua kama bidhaa.

“Kama nina mtu wangu nampenda na yeye ananipenda kwa nini tusikubaliane tu wazazi wakatutambua, na ikifika hatua ya kufunga ndoa mahari yangu nataka bei ya kawaida tu maana wengine hata elfu thelathini anaolewa na anaishi vizuri lakini sio kila kukicha mtu anakufanyia vitendo vibaya ndani ukimuuliza anakuambia kakutolea mahari kubwa, mimi hiyo sitaki hata elfu hamsini naolewa tu,” alisema Poshy.

Post a Comment

1 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Mie itabidi nizungumze na mzee Obeid ili tuingie katika mchakato wa Mahari halisi ngombe si chini ya 48 nimeziweka tayari na mbili baada ya Mauidi ya ndoa Mashallah umeubika mtoto.

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad