Rapa maarufu hapa nchini ambaye pia ni Mbunge wa Mikumi, Joseph Haule ‘Prof. Jay’, ameibuka na kuikanusha vikali taarifa ya Chama cha Hakimiliki Tanzania (The Copyright Society of Tanzania – COSOTA) kwamba wamemsimamia na kuhakikisha amelipwa pesa zake Tsh. milioni 100, kutoka nchini Uganda.
Kupitia ukurasa wake wa Twitter, Prof. Jay amewataka COSOTA kuweka rekodi sawa kwani hajapewa pesa hizo yeye, bali alilipwa mwandaaji wa kazi za muziki, prodyuza Majani ‘P Funk’, kwa kutumia ‘melody’ ya wimbo wa NIKUSAIDIEJE ulioimbwa na Prof J na Majani akiwa prodyuza.
Hata hivyo, baada ya kauli hiyo ya Prof Jay, P Funk Majani alionekana kupandwa na hasira na kuamua kumpa Makavu Prof. Jay kwa kudai kuwa ni mlafi na anaroho mbaya.