Putin Aiomba Marekani Kuanzisha Mazungumzo ya Nyuklia

Putin Aiomba Marekani Kuanzisha Mazungumzo ya Nyuklia
Rais Vladimir Putin wa Urusi hii leo ameiomba Marekani kuanza mazungumzo mapya baada ya kuvunjika kwa makubalino ya nyuklia yaliyofikiwa baada ya kumalizika kwa Vita Baridi kati ya mataifa hayo yenye nguvu duniani. 

Putin amenukuliwa kwenye taarifa yake akisema ili kuzuia machafuko yasiyo na msingi, mipaka na sheria, Marekani inahitaji kwa mara nyingine kupima uwezekano wa athari mbaya na kuanza mazungumzo bila ya masharti yoyote, na Urusi iko tayari kwa hilo. 

Urusi inailaumu Marekani kwa kuuvunja mkataba wa nyuklia wa INF uliofikiwa mwaka 1987 baada ya wakuu wa nchi wakati huo - Ronald Reagan wa Marekani na Mikhail Gorbachev wa Muungano wa Kisovieti - kutiliana saini. Putin ameonya iwapo Urusi itapata taarifa za Marekani kutengeneza makombora mapya, nayo pia italazimika kuanza kutengeneza kikamilifu makombora kama hayo.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad