R Kelly Hatarini Kufungwa Miaka 195

R Kelly Hatarini Kufungwa Miaka 195
Mwanamuziki RKelly huenda akakutana na kifungo cha miaka 195 jela baada ya jana kufikishwa mahakamani, akituhumiwa makosa 13 yanayohusiana na unyanyasaji wa kingono, ambapo amepangiwa kurudi tena mahakamani Septemba 14, 2019.


RKelly amepandishwa kizimbani siku ya jana katika Mahakama ya Brooklyn ili kutetea kesi hizo zinazomkabili zikiwemo kunyanyasa, kudhalilisha, na kushambulia wanawake kingono pamoja na kuwarekodi watoto wadogo picha zisizokuwa na maadili.

Baada ya kupandishwa kizimbani siku ya jana Shirikisho la Mahakama na waendesha mashtaka wa kesi hiyo, ambapo wamesema R.Kelly atarudi tena mahakamani Septemba 14, kama akikutwa na hatia atapata adhabu ya kifungo cha miaka 195 jela.

R.Kelly kwa sasa amerudishwa mahabusu na wanasheria wake wamesema mteja wao amenyimwa haki kutokana ya kutopewa dhamana.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad