Rais Dkt. John Mpombe Magufuli amekabidhiwa rasmi Uenyeketi wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini Mwa Afrika (SADC), ambapo mkutano wa SADC unafanyika nchini Tanzania kwa siku mbili ukiwa umehudhuriwa na Marais 11 kutoka nchi mbalimbali wanachama wa SADC.
Akifungua mkutano huo ambao umehudhuriwa na Marais 11 kutoka nchi mbalimbali wanachama wa SADC Rais Magufuli amesema ni fursa nzuri kwa Watanzania kuendelea kulitangaza taifa kupitia mkutano huu wa kihistoria.
Dkt Geingob amesema mafanikio ya viwanda ni dira nzuri kwa maendeleo na mfano wa kuigwa kwa nchi wanachama Jumuiya ya SADC hivyo ni fursa nyingine kwa kujifunza kwa Tanzania huku Mwenyekiti huyo aliyemaliza muda wake akitangaza Kiswahili kuwa lugha ya nne inayotumika kwenye vikao mbalimbali vywa jumuiya hiyo.
Rais Magufuli akabidhiwa rasmi Uenyekiti SADC, Kiswahili ruksa kutumika kwenye jumuiya hiyo
0
August 17, 2019
Tags