Rais John Magufuli leo Alhamisi Agosti Mosi, 2019, anatarajia kufungua rasmi Uwanja wa Ndege wa Julius Nyerere jengo la Terminal 3, ambao upanuzi wake ulianza 2013 na kugharimu Sh788.6 bilioni
Mradi huo ulianza kujengwa 2013 na awali ulipangwa kutekelezwa kwa Sh705.3 bilioni lakini kutokana na kubadilika kwa taratibu za kikodi, mchoro wa mradi (Design) na gharama ya mradi huo iliongezeka kwa Sh85.3 bilioni.
Kampuni iliyotekeleza mradi huo ni BAM International ya Uholanzi ambayo ndiyo iliyofanya kazi za kikandarasi na Arab Consulting Engineers (ACE) ya Misri, ilifanya kazi za ushauri.