Rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa Asema Morogoro ni Nyumbani Kwetu

Rais wa Afrika kusini Cyril Ramaphosa ametembelea kambi ya Mazimbu mkoni Morogoro eneo ambalo mamia ya wapigania uhuru toka Afrika Kusini waliishi na na kufanyia mafunzo wakati wa ubaguzi wa rangi.

Akishukuru Ramaphosa amalitaja eneo hilo kuwa Macca ya harakati za ukombozi wa Afrika kusini na kuwashukuru ndugui zao watanzania kwa msaada wao wa hali na mali katika kipindi hicho kigumu katika historia ya taifa lao

Eneo hilo lilitolewa kwa Afrika Kusini na muasisi wa Taifa la Tanzania hayati mwalimu Julius Kambarage Nyerere na sasa liko chini ya uangalizi wa Chuo Kikuu cha Kilimo Sokoine kilichopo mkoani Morogoro.


Ramaphosa amesema eneo hilo ni muhimu kwake binafsi kwani sehemu ya familia yake imeishi kwenye kambi hiyo kwa muda mrefu.

"Watoto wawili wa kaka yangu wamezaliwa hapa, hivyo eneo hili ni sehemu ya maisha yangu milele kwasababu vitovu vyao vilizikwa hapa," amesema Ramaphosa.

Ramaphosa pia aliembelea eneo la makaburi ambapo baadhi ya wapigania uhuru hao walizikwa: "eneo hili wamezikwa watu waliokuja kutoka Afrika Kusini na wengine walizaliwa hapa kwa ajili ya kupigania uhuru, tunawashukuru watu wa Morogoro kwa ushirikiano mliowapa walioishi hapa."

Pia ameiomba serikali ya Tanzania kufikiri namna ya kuliendeleza eneo hilo kuwa kivutio cha utalii kwa siku za usoni.

Ramaphosa yuko Tanzania kwa ajili mkutano wakuu wa nchi wanachama wa Jumuiya ya Mendeleo ya Kusini mwa Afrika ambao utafanyika mwishoni mwa juma jijini Dar es salaam.

Tayari wakuu kadhaa wa mataifa hayo wameshawasili jijini Dar es Salaam kwa ajili ya mkutano huo.

Rais Mwenyeji John Magufuli wa Tanzania atachukua kijiti cha kuiongoza jumuiya hiyo kwa mwaka mmoja toka kwa Mwenyekiti wa sasa Rais wa Namibia Hage Geingob.

Post a Comment

2 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Alichosema Ramphosa ni kweli. Tumeishi nao Kindugu na chetu kilikuwa ni Chao kwa ukarimu wetu.

    Na tusipo waona kwa sikumbili tatukama hawakuja nyumbani basi huwa tunawafata kwenda kuwatembelea na kuwajulia hali na kila jumamosi tunakwenda kucheza nao mpira kuongeza sirikiao na urafiki wa karibu na udugu.

    Dzliamini alitoa mimba zangu tatu kwa kuogopa kuzaa na sheria zilizo kuweo wakati ule kambini hapo.

    Ni kweli ni laziima hili eneo lienziwe na lipewe Kigwagalla akishiikia na na serikali ya Sauzi chiniya Wizara husika na chini ya mfuko wao ambapo Tanzania baadae atakuwa ni muangalizi naa muendeshaji na wakati ndio huukwa mataifa yote. Hawa walio wacha vitovu vyao hapa ni kweli usiopingika walipata Amani na USalama na waliku kwa ndugu Zao.

    ReplyDelete
  2. Agwe muwaha ..!!! Kabudi Milimonyi...!!
    Challenge yetu na Mkulu ni even lesser than mwalimu path way.
    Ikiwemo Kuhakikisha ndugu zetu wa Zimbabwe vikwazo wanaondolewa mara moja we start lobbying now and Mobilisation.
    Sarah Cookie tunae naalifaya megi mazuri Bangladesi na ni muelewa na as dynamic as you.

    Tuwa dhihirishie Tanzania was not only Mwalimu but its in our DNA.

    ALE WAZELELO MLUNGU AWATA'ZE
    UMLMSA'JE JEEMDALLI MAGUFULI.

    UMLONJE'LEE MILIMO ILIBAHO MISWAO DUU.

    HAPA KAZI TU.

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad