Rais wa Brazil aamuru majeshi kushiriki kuzima moto katika msitu wa Amazon


Rais wa Brazil, Jair Bolsonaro, ameamuru majeshi kushiriki katika operesheni ya kuzima moto katika msitu wa Amazon, siku moja baada ya wanaharakati wa mazingira kulaumu serikali yake kwa kuwahamisha wakulima kuandaa mashamba suala lililosababisha moto huo.

Moto wa msituni hutokea kipindi cha ukame na jua kali, lakini pia inawezekana na matokeo ya shughuli ya kusafisha ardhi kwa ajili ya kilimo na ufugaji.

Kwa mujibu wa shirika la kimazingira WWF, msitu wa Amazon unazalisha asilimia 20 ya maji safi ya Duniani. Amazon pia inakaliwa na viumbe zaidi ya milioni 3, wanyama na mimea pamoja na wakazi wa asili ya eneo hilo milioni moja.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad