RC apiga marufuku watumishi kwenda likizo
2
August 17, 2019
Mkuu wa Mkoa wa Lindi, Godfrey Zambi amepiga marufuku watumishi wa Serikali kwenda likizo kwa muda wa miezi mitatu, ili kusimamia miradi ya Maendeleo na vitambulisho vya wajasiriamali kwenye maeneo yao, na maandalizi ya mapokezi na uzimaji wa Mwenge wa Uhuru.
Ameweka zuio hilo alipokuwa anazungumza katika kikao kazi na watumishi mbalimbali, wakiwemo Ma Ofisa Tarafa na watendaji Kata wa Halmashauri za Wilaya na Manispaa ya Lindi kilichofanyika uwanja wa Ilulu mjini humo.
Amesema kuwa amechukua uamuzi huo kufuatia Shughuli nyingi inazoukabiri Mkoa huo kwa mwaka huu, kama vile uzimaji mwenge wa Uhuru utakaohitimisha mbio zake na kumbukizi za kifo cha hayati Baba wa Taifa, Mwalimu Julius K. Nyerere Oktoba 14 mwaka huu na haraiki ya vijana.
Aidha, amesema kuwa kutokana na majukumu hayo, amelazimika kuzuia watumishi wote wa Serikali, Wakiwemo Wakuu wa Wilaya, Wakurugenzi Watendaji wa Halmashauri za Wilaya na Manispaa, Ma-Ofisa Tarafa, watendaji Kata, vijiji, Mitaa na vitongoji kutoenda likizo, kwa muda hadi pale zitakapokamilika shughuli hizo.
Zambi amezitaja sababu nne, ikiwemo ujio wa Mwenge wa Uhuru, kufuatilia utekelezaji wa miradi ya maendeleo, shughuli za vijana na ukamilishaji wa zoezi la uuzwaji wa vitambulisho vya wajasiriamali.
“Kuanzia leo nazuia likizo zote za watumishi wote wa Serikali hadi mwezi Disemba mwaka huu,”amesema Zambi.
Hata hivyo, Mkuu huyo wa Mkoa amesema kuwa Mkoa una miradi mingi, kama vile ujenzi wa vituo vya Afya, Zahanati na Shule lakini kutokana na kukosa usimamizi wa karibu imekuwa ikilegalega utekelezaji wake.
Tags
Sheria ya kazi juu ya likizo kwa mwajiriwa yasemaje? Si haki kwa mfanyakazi kwenda likizo?
ReplyDeleteUko sahihi, wafanyakazi wassiomaliza kazi zao kwa muda uliotaraiwa ni kwamba wana changamoto ikiwemo uzembe, kwa hiyo kusitisha likizo ili kumalizia kazi viporo nijabola kawaida na kuongeza masaa ya kazi pia ni utatuzi japokuwa hali haipendwi na watumisi waajiriwa.
ReplyDeleteKusitisa Likizo kwa muda ni Haki ya Muajiri pale inapo bidi na ndicho kilicho fanyika hapa to achieve and clear the backlog of non performer.
Badilikeni kuendana na kasi ya Awauya Tano. Tena mna bahati.ingekuwa ktk halmashauri yetu ningewashusha ngazi
Hapa Kazi Tu.