Mwanamuziki na mfanyabiashara duniani Rihanna, amemtolea uvivu Rais wa Marekani Donald Trump, kwa kutochukua hatua yoyote baada ya kutokea shambulio la kigaidi nchini humo.
Rihanna aliandika kupitia ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa Instagram kuwa, "yametokea matukio mawili ya kigaidi kwenye nchi yako, watu karibia 30 wasio na hatia wamepoteza maisha, sasa hivi imekuwa rahisi mtu kununua silaha kama AK-47 ili akafanye shambulio kuliko kupata Visa''.
Rihanna aliendelea kuandika kuwa Dunia inaifikiria Marekani ndio Nchi inayoonekana kufuga magaidi na majambazi kutokana matukio yaliyotokea wikiendi hii.
Siku ya Jumamosi na Jumapili watu 29 walifariki dunia kwa matukio tofauti ya kushambuliwa kwa risasi katika miji ya California na Texas, lakini hadi sasa Donad Trump hajachukua hatua yoyote zaidi ya kutoa pole kwenye mtandao wa Twitter.
Ndani ya mwaka huu pekee nchini Marekani watu 293 wameuwa kwa shambulio la risasi, na jumla ya watu 1072 wamejeruhiwa kwa shambuli hilo.