Robert Mugabe aendelea kupatiwa matibabu kwa miezi mitatu sasa


Imeelezwa kwamba Rais wa zamani wa Zimbabwe, Robert Gabriel Mugabe, 95 amekua akipatiwa matibabu nchini Singapore kwa zaidi ya miezi mitatu huku hali yake ikielezwa kuendelea kuimarika.

Taarifa ya Rais Emmerson Mnangagwa haikubainisha ni nini hasa Mzee Mugabe amekua akitibiwa ughaibuni licha ya fununu za kuandamwa na magonjwa ya uzeeni.

Mugabe alitawala nchi hiyo tangu uhuru wake mwaka 1980 hadi alipopewa shinikizo la kujiuzulu na jeshi la ukombozi la nchi yake mwaka 2017.

Imeelezwa kwamba umekua ni utaratibu wa kawaida kwa kiongozi huyo wa zamani aliojiwekea wa kupatiwa matibabu nchini Singapore kwa zaidi ya miaka 10.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad