Sakata la Korosho..Serikali Yakiri Kudaiwa Bilioni 95 na Wakulima
0
August 30, 2019
Waziri wa Kilimo, Japhet Hasunga amesema matarajio yao walipoenda kulipa Wakulima walidhani ni fedha kidogo ila walipoingia kwenye utekelezaji walikuta wanatakiwa kulipa Tsh. Bilioni 723 ambazo ni fedha kubwa kwa nchi yetu
Amesema, Serikali ilijitahidi kutafuta fedha na kuiagiza Benki ya Kilimo kutoa mkopo kwa Bodi ya Nafaka ambapo Bodi hiyo iliweza kulipa Tsh. Bilioni 650 na kati ya hizo Tsh. Bilioni 630 zimelipwa moja kwa moja kwa Wakulima na nyingine zikilipia maghala na wasafirishaji
Amebainisha hadi sasa ana uhakika Wakulima wanadai Tsh. Bilioni 95 lakini ukichanganya na Wadau wengine kama Wasafirishaji, Maghala na Vyama vya Ushirika, Serikali inadaiwa Tsh. Bilioni 105
Aidha, amefafanua kuwa Wakulima wanaodai hadi sasa ni Wakulima wakubwa wanaozalisha kuanzia kilo 1500 na kuendelea, Wakulima wadogo kwa asimilia 99 wameshalipwa madai yao
Kuhusu maandalizi ya msimu ujao amesema Wakulima wakubwa wamelipwa kwa asilimia 30 ili waweze kuandaa mashamba huku wakisubiri asilimia 70 lakini pia Serikali inawakopesha wakulima pembejeo kwa aslimia 50 ambapo wao hulipia asilimia 50 iliyobaki
Aidha, amebainisha kuwa hadi sasa Serikali ina korosho tani 200,000 kwa ajili ya kuziuza nje ya nchi na kwa hatua iliyopo sasa Korosho hizo zote zitanunuliwa na viwanda kutoka Vietnam
Tags