Sanchi: Kwa siku natongozwa zaidi ya mara 100


BAADA kukaa kimya kwa muda mrefu ingawaje anakutana na vishawishi vingi, mwanamitindo mwenye umbo tatanishi, Jane Rimoy ‘Sanchi’ ameamua kufunguka kuwa anapata shida mitandaoni ambapo kwa siku anatongozwa zaidi ya mara 100.



Akizungumza na Za Motomoto ya Risasi, Sanchi alisema kuwa watu wasichokijua ana mtu wake lakini anakutana na usumbufu sana kwenye ukurasa wake wa Instagram (DM) kwa kupokea meseji za kutongozwa zaidi ya 100.

“ Unajua mtu akikuona kwenye mitandao vile anakuona anaweza kukupata kirahisi kumbe sivyo, kwanza mimi sitaki usumbufu jamani wajue na mimi ni mwanamke wa mwenyewe, wasichukulie maisha yangu ya mtandao ndiyo maisha halisi wajifunze hilo,” alisema Sanchi

Post a Comment

1 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Tunaomba ufafanuzi wa siku.
    ili itusaidie kupiga mahesabu kuweza kuangalia kipato chako katika mwaka TRA tuweze kufanya makadirio Rafiki kwa Dau Poa.
    haraka kwa siku 100x200000=20000000
    20000000x30=6000000000 kwa mwezi
    600000000x12= ( Nisaidieni jibu wadau)

    Kumbe inalipa.

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad