Sanders Amtuhumu Trump kwa Mauaji ya El Paso

Sanders Amtuhumu Trump kwa Mauaji ya El Paso
Mgombea wa urais wa chama cha Democrat nchini Marekani Bernie Sanders amemtuhumu Rais Donald Trump kwa kutengeneza mazingira ya uaudui na chuki ambayo huenda ndio yaliyomvutia mshambuliaji aliyewaua watu 20 katika jimbo la Texas. 

Seneta Sanders anayepigiwa chapuo katika kinyang'anyiro cha kumkabili Rais Trump kwenye uchaguzi wa 2020 alimkosoa vikali Rais Trump wakati alipozungumza na kituo cha televisheni cha Marekani cha CNN hapo jana. Alisema ni wazi Rais Trump hapendelei mtu yeyote kuwaua watu wasio na hatia, lakini hatua yake ya kuwalinganisha wahamiaji na watu wasiokuwa 

Wazungu kama wavamizi huenda imesababisha wafuasi wake kuchukua hatua kama hiyo. Alisema viashiria vyote vinaonesha kwamba Marekani ina rais mbaguzi wa rangi anayejaribu kuwaridhisha wanaopendelea siasa za uzalendo wa watu weupe.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad