Saudi Arabia: Wanawake sasa ruksa kusafiri nje ya nchi,
0
August 02, 2019
Wanawake nchini Saudi Arabia sasa wanaweza kusafiri nje ya nchi bila kusindikizwa na wanaume, limesema agizo la ufalme.
Dalia Yashar is one of the first Saudi students to register to become a commercial pilot [Hamad Mohammed/Reuters]
Chini ya sheria mpya iliyotangazwa siku ya Ijumaa, mwanamke mwenye umri wa miaka zaidi ya 21 anaweza kutuma maombi ya paspoti bila idhini ya mlezi wa kiume.
Watu wazima wote wanaweza sasa kuomba paspoti na kusafiri hatua inayowapatia haki sawa na wanaume. Agizo hilo la ufalme pia linawapa wanawake haki ya kuwasajili watoto wao wanapojifungua, kufunga ndoa au talaka.
Kwa mujibu wa shirika la habari la BBC, Pia sheria hiyo mpya inazungumzia sheria za ajira ambazo zinapanua fursa kwa wanawake. Kwa mujibu wa sheria hiyo, raia wote wana haki ya kufanya kazi bila kukabiliwa na ubaguzi wowote kwa misingi ya jinsia, ulemavu au umri.
Wanawake wa Saudia wamekuwa wakiomba ruhusa kutoka kwa mwanaume mlezi wa kiume, Mme , baba au ndugu mwingine wa kiume kuomba paspoti
Hadi sasa, wanawake wa Saudia wamekuwa wakiomba ruhusa kutoka kwa mlezi wa kiume, Mumewe , baba au ndugu mwingine wa kiume kuomba paspoti ama kibali chochote cha kusafiri nje ya nchi.
Wanawake wa Saudi ArabiaWanawake wa Saudi Arabia
Mtawala wa Saudia Mwanamfalme Mohammed bin Salman amelegeza masharti katika nchi hiyo kama vile kumzuwia mwanamke kuendesha gari kama sehemu ya juhudi kubwa za kufungua taifa hilo.
Mwaka 2016, alifichua mpango wa kufanya mageuzi ya kiuchumi ifikapo 2030, kwa lengo la kuongeza ushiriki wa wamawake kwa 30% kutoka 22%.
Hata hivyo kumekuwa na kesi kubwa za wanawake wanaotaka uhamiaji katika nchi kama vile Canada, kutokana na madai ya unyanyasaji wa kijinsia wakidai.
Mnamo mwezi January, Canada ilimpa hifadhi ukimbizi msichana Rahaf Mohammed al-Qunun mwenye umri wa miaka 18. Aliikimbia Saudi Arabia na kujaribu kutorokea nchini Australia. Alisababisha hali ya sintofahamu katika chumba cha hoteli iliyopo katika uwanja wa ndege katika mji mkuu wa Thailand Bangkok, ambako alikuwa akiomba msaada wa kimataifa.
Mashirika ya kimataifa mara kwa mara yamekuwa yakidai kwamba wanawake wanachukuliwa kama raia wa daraja la tatu nchini humo.
Tags