Serikali haitavumilia taasisi itakayokwamisha juhudi zake- Kangi Lugola


Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola, amesema kuwa Serikali ya Tanzania haitavumilia taasisi yeyote ambayo itaonyesha nia ya kukwamisha zoezi la kuwarejesha wakimbizi, wanaotokea nchi jirani ya Burundi.

Lugola ametoa kauli hiyo akiwa mkoani Kigoma alipotembelea kambi ya Wakimbizi Nduta, iliyopo wilayani Kibondo mkoani humo akiwa na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Burundi.

“Wakimbizi wa Burundi wanaoishi Tanzania, wanalelewa vizuri sana na mpango wa Serikali ni kuwarejesha nyumbani kwao Burundi, kwa kuwa sasa kuna amani.”amesema Lugola

Aidha, Waziri Lugola amesema Serikali katika kila wiki itakuwa ikiwarudisha wakimbizi 2000 mpaka pale watakapoisha.
Tags

Post a Comment

1 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Ninja bila kumsahau Msaliti WA Uvira panga pangua na yeye pia awepo KATIKA list ya watakao rudishwa.

    Alipataje kuingia KATIKA combo Cha kuunga sheria mpaka kuwa KATIKA kamati Za bunge na sasa baada ya kufukuzwa CDM kaanzisha Act.

    Ninja Wana Kigoma na sisi pia hatumtaki mleta mtafaruku WA Nyakabiga. Rudishwa kwao

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad