Serikali ya Uingereza yamuomba Malkia Elizabeth asimamishe bunge kwa muda


Malkia Elizabeth ameombwa na serikali kuvunja bunge siku chache tu baada ya wabunge kurejea kazini mwezi Septemba - na wiki chache kabla ya muda wa mwisho ambao Uingereza ilipewa kuondoka kwenye Jumuiya ya Ulaya (EU) maarufu kama Brexit.

Mhariri wa masuala ya siasa wa BBC Laura Kuenssberg anasema kuwa hatua hii itatoa fursa kwa utawala mpya wa Waziri Mkuu Boris Johnson kuandaa hotuba ya Malkia - ukiainisha mipango ya serikali - tarehe 14 Oktoba.

Lakini ina maana kuwa wabunge huenda wasiwe na muda wa kupitisha sheria yoyote inayoweza kumzuia Waziri Mkuu kuiondoa Uingereza nje ya EU bila mkataba tarehe 31 Oktoba.

Wabunge wasiokuwa na madaraka au nafasi yoyote serikalini na mwanakampeni aliyesalia Dominic Grieve wamekiita "kitendo hicho kuwa kisichokubalika", wakaonya kuwa kinaweza kusababisha kupigiwa kwa kura ya kutokuwa na imani dhidi ya Bwana Johnson, akiongeza kuwa "Serikali hii itaanguka."


Lakini chanzo kutoka ofisi ya Waziri Mkuu kilitetea uamuzi huo , kikisema: "Ni wakati muafaka kwa serikali mpya na waziri mkuu kuweka mipango kwa ajili ya nchi kabla hatujaondoka katika Muungano wa Ulaya ."

Wazo la kusimamisha kazi za bunge bila kulivunja - limesababisha utata, huku wakosoaji wakisema litawazuwia wabunge kuweza kutekeleza wajibu wao wa kidemokrasia katika mchakato wa Brexit.

Viongozi wenye sifa kubwa katika siasa za Uingereza, akiwemo waziri Mkuu wa zamani wa Uingereza John Major, wametishia kwenda mahakamani kuzuwia wazo hilo.

Upinzani, ukiongozwa na msemaji wa chama cha kitafa cha Uskochi SNP - ambacho hakipendelei kujiondoa katika Muungano wa Ulaya Joanna Cherry tayari anajiandaa kwenda katika mahakama za Uskochi kupinga hatua hiyo.

Laura Kuenssberg amesema ni idadi ndogo tu ya mawaziri katika serikali waliofahamu mapema kuhusu mpango na kwa hiyo italeta mzozo mkubwa.

Amesema serikali itadai kuwa ulikuwa ni "mfano wa kiwango cha mchakato wa hotuba ya Malkia," licha ya kelele zinazozingira.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad