TAKUKURU yamdaka Mwenyekiti wa CCM wa Kata

Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) Mkoani Lindi imemkamata na kumfikisha Mahakamani Mwenyekiti wa CCM Kata ya Likongowele, wilaya ya Liwale, Mohamed Ndope kwatuhuma za kuomba na kupokea rushwa.

Akizungumza na waandishi wa habari mjini Lindi, Kaimu Mkuu wa TAKUKURU wa Mkoa wa Lindi, Noel Mseo alisema mwenyekiti huyo ambae pia ni mjumbe wa kamati ya siasa ya Chama Cha Mapinduzi ( CCM) wilaya ya Liwale alikamatwa 28/7/2019 saa moja jioni, mtaa wa Nangando, mjini Liwale.  Kwatuhuma za kuomba rushwa ya shilingi 300000 toka kwa mtumishi wa idara ya afya katika wilaya ya Liwale.

Mseo ambae aliweka wazi kwamba Ndope alikamatwa akiwa na fedha taslimu shilingi 300,000 alisema Ndope ambae tayari amefikishwa katika mahakama ya wilaya ya Liwale aliomba na kupokea rushwa kwa mtumishi huyo.

''Kutoka tarehe 24.7.2019 alikuwa kupewa kiasi hicho cha fedha kutoka kwa mtumishi huyo, akidai kwamba angeweza kumsaidia asichukuliwe hatua. Nikufuatia malalamiko ya wananchi kwa mtumishi huyo ambae ni muuguzi,'' alisema Mseo.

Ofisa huyo mwandamizi wa TAKUKURU alisema taasisi ilipopata taarifa yakuwepo mazingira ya kada huyo wa CCM kuomba rushwa ilianza kufuatilia na kubaini kwamba  Ndope alikuwa anashawishi kupewa rushwa.

Ndipo ilipoweka mtego, nakufanikiwa kumtia mikononi. Kwamujibu wa Mseo, mtuhumiwa huyo jana alifikishwa katika mahakama ya wilaya ya Liwale.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad