TAKUKURU Yampandisha Mahakamani Mwenyekiti wa CCM

TAKUKURU Yampandisha Mahakamani Mwenyekiti wa CCM
Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU), Wilaya ya Liwale, Mkoani Lindi, imemfikisha mahakamani Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Kata ya Likongowele, Mohamedi Ndope akidaiwa kuomba na kupokea rushwa ya Sh. laki 3.


Akimsomea shitaka lake Mwanasheria wa TAKUKURU mkoani Lindi, ameeleza mshitakiwa alikamatwa eneo la Nangando, Liwale Mjini, Julai 28, 2019 majira ya saa 3:00 usiku, akipokea kiasi hicho cha fedha kutoka kwa mlalamikaji ambaye ni mtumishi wa Idara ya Afya.

Mwasheria huyo wa TAKUKURU amedai mahakamani hapo mtuhumiwa aliomba rushwa hiyo kutoka kwa mtumishi wa Afya, ili kumsaidia asichukuliwe hatua za kinidhamu kufuatia uwepo wa malalamiko kutoka kwa baadhi ya wananchi.

Ameendelea kusema, kutokana na kitendo hicho mshtakiwa akiwa ni kiongozi wa chama ambacho kinapinga masuala ya rushwa, amefanya kosa kwa mujibu wa kifungu cha 15 cha Sheria ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Namba 11/2007.

Hata hivyo mshtakiwa amekana kosa linalomkabili na yupo nje kwa dhamana, na kesi yake imepangwa kusikilizwa tena Mahakamani hapo Agosti 15, 2019.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad