Timu ya Yanga Kutua Dar Leo Wakitokea Moro


JESHI zima la kikosi cha Yanga leo mchana linatarajiwa kutua jijini Dar likitokea mkoani Morogoro lilipoweka kambi yake kwa ajili ya kusubiri kuvaana na Kariobangi Sharks katika kilele cha Wiki ya Mwananchi huku likitarajiwa kupokelewa kwa kishindo kutokana na maandalizi waliyoandaliwa.



Yanga walijichimbia Morogoro kwa takriban mwezi mmoja wakiwa wameweka kambi ya kujiandaa na msimu ujao wa Ligi Kuu Bara pamoja na Ligi ya Mabingwa Afrika.



Kikosi hicho kinatua leo mchana kwa ajili ya kuhitimisha Wiki ya Mwananchi ambapo watapokelewa mkoani Kibaha ambapo wameandaliwa mapokezi maalum.



Akizungumza na Championi Ijumaa, Mratibu wa Yanga, Hafidh Saleh amesema watatua jijini Dar mchana kutokana na asubuhi kuwa na programu ya mazoezi ya mwisho. “Mambo yote yako vizuri hapa Morogoro na tumeshakamilisha kambi yetu ambapo kesho (leo) Ijumaa tutafanya mazoezi ya mwisho kabla ya kuondoka.



Tulimaliza kambi yetu kwa kucheza mechi ya mwisho na Friends Rangers na hatutacheza tena hadi katika Wiki ya Mwananchi. “Tunamalizia programu ya mwalimu asubuhi kisha mchana tunafanya safari ya kuja Dar. Kila kitu kimeenda vizuri na uzuri ni kuwa hakuna majeruhi.



“Mara baada ya kufaika Dar, tutakuwa tunajiandaa na mchezo wetu dhidi ya Kariobangi Sharks katika kilele cha Wiki ya Mwananchi,”

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad