Timu za Ligi kuu kupunguzwa, huu ndio mpangilio

Bodi ya Ligi (TPLB) imetangaza mabadiliko ya kanuni za Ligi kuu, ikiwemo kupunguza timu kutoka 20 hadi 16 ifikapo msimu wa 2021/22.


Timu nne msimu huu (2019/20) zitashuka daraja moja kwa moja yaani aliyeshika nafasi ya 17/18/19/20 anashuka moja kwa moja kwenda ligi daraja la kwanza huku aliyeshika nafasi ya 15/16 atacheza Play Off na timu za ligi daraja la kwanza.

Msimu wa 2020/21 ligi kuu itashirikisha timu 18 ikiwa timu 14 zilizobaki ligi kuu, timu 2 ambazo zimepanda daraja moja kwa moja kutoka ligi daraja la kwanza na timu 2 washindi wa jumla wa Play Off ya timu zilizoshika nafasi ya 15/16 ligi kuu na washindi wa jumla wa Play Off ya ligi daraja la kwanza.

DARAJA LA KWANZA

Msimu huu (2019/20) zitashuka timu 8 moja kwa moja ikiwa timu 4 kila kundi timu ambazo zimeshika nafasi ya 9/10/11/12 kwenye kundi, itashuka moja kwa moja kwenda daraja kwa pili huku aliyeshika nafasi ya 7/8 atacheza play off  na timu za daraja la pili.

Timu ilishika nafasi ya kwanza kwenye kundi itapanda ligi kuu moja kwa moja huku timu ambayo imeshika nafasi ya 2/3 kwenye kundi A itacheza play off na timu iliyoshika nafasi ya 3/2 kwenye kundi B. Mshindi wa jumla hapo atacheza play Off ya kupanda ligi kuu au kubaki ligi daraja la kwanza na timu zilizoshika nafasi ya 15/16 kwenye ligi kuu.

Timu zilizoshika nafasi ya 7/8 kwenye kundi A zitacheza Play Off na timu zilizoshika nafasi ya 8/7 kwenye kundi B na aliyefungwa atacheza play Off ya kubaki ligi daraja la kwanza au kushuka daraja la pili na timu ambazo zimefika hatua ya nusu fainali ya sita bora ya ligi daraja la pili.

Msimu wa (2020/21) ligi daraja la kwanza zitashiriki timu 20 ikiwa timu 12 zilizobaki ligi daraja la kwanza (6 kila kundi), timu 4 ambazo zimeshuka daraja kutoka ligi kuu, timu 2 ambazo zimepanda daraja kutoka ligi daraja la pili na timu 2 ambazo zitashinda michezo ya play Off kwa timu zilizoshika nafasi ya 7/8 na zile mbili kutoka ligi daraja la pili.

LIGI DARAJA LA PILI

Msimu huu (2019/20) zitashuka timu 12 kutoka kwenye makundi 3 ya ligi daraja la pili ikiwa timu 4 kila kundi timu iliyoshika nafasi ya 5/6/7/8 kwenye kundi itashuka moja kwa moja kwenda ligi daraja la tatu (Mabingwa wa mikoa). Na timu 2 kila kundi ambazo zitashika nafasi 2 za juu kwenye kundi A,B,C zitafuzu hatua ya sita bora.

Kutakuwa na fainali ya sita bora kwa ligi daraja la pili timu 2 kutoka kila kundi zitapangwa makundi mawili yenye timu 3 kila kundi na zitacheza mechi kwenye kituo kimoja timu ambayo imeshika nafasi ya 1/2 kwenye kundi A na B zitafuzu hatua ya nusu fainali.

Timu ambazo zitashinda hatua ya nusu fainali zitakuwa  zimepanda moja kwa moja ligi daraja la kwanza na timu ambazo zimefungwa zitacheza michezo ya play off na timu ambazo zimefungwa michezo yake ya play off ya ligi daraja la kwanza kwa walioshika nafasi ya 7/8.

Msimu wa 2020/21 ligi daraja la pili litashirikisha timu 20 ikiwa timu 8 zilizobaki ligi daraja la pili timu 8 zilizoshuka kutoka ligi daraja la kwanza na timu 2 zilizopanda kutoka ligi daraja la tatu (Mabingwa wa mikoa) na timu 2  ambazo zimeshindwa michezo ya play Off  ya timu za ligi daraja la kwanza na timu za daraja la pili zilizofika nusu fainali.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad