Tundu Lissu atua mahakamani kupigania ubunge wake


Dar es Salaam. Mbunge wa zamani wa Singida Mashariki, aliyevuliwa wadhifa huo hivi karibuni, Tundu Lissu ameanza rasmi harakati za kupigania ubunge wake mahakamani baada ya kufungua shauri la maombi ya kibali cha kupinga uamuzi huo wa kumvua ubunge.

Mwanasheria huyo mkuu wa Chadema ambaye yuko nchini Ubelgiji alikokuwa akipatiwa matibabu baada ya kushambuliwa kwa risasi na watu ambao hadi sasa hawajajulikana, alifungua rasmi shauri hilo jana.

Lissu ambaye pia alikuwa Mnadhimu Mkuu wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni, amekuwa nje ya nchi kwa matibabu baada ya kunusurika katika jaribio hilo la mauaji lililotokea Septemba 7, 2017 akiwa nje ya makazi yake huko Dodoma.

Amefungua shauri hilo chini ya hati ya dharura, kupitia kwa kaka yake Alute Mughwai ambaye amempa mamlaka ya kisheria kufanya hivyo.

Uamuzi wa kumvua Lissu ubunge ulitangazwa na Spika wa Bunge, Job Ndugai Juni 28, wakati akiahirisha mkutano wa 15 wa Bunge, huku akitaja sababu mbili.

Alizitaja sababu hizo kuwa ni kushindwa kuhudhuria vikao vya Bunge kwa muda mrefu bila kumjulisha Spika kwa maandishi mahali aliko na sababu ya pili ni kutokujaza taarifa za mali na madeni kwa mujibu wa Sheria ya Maadili ya Viongozi wa Umma.

Mwananchi
Tags

Post a Comment

3 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Lizzu, Napenda kukumbusha kwamba, kama
    ulidani na kujiaminisha katika kichwa chako (abacho sina uhakika wa afya yake kama ni timamu) kwamba ni kazi. La hasha. Ubunge ni uwakilishi.
    Na ukipoteza sifa na vigezowala usitafte timbwili za kuwamitandaoni na magazeti. kutafuta Kiki na kama ulivyo zoea ile Tanzania ya miakka ile.
    Hii ni Tanzania mpya na sisi waaHabari tutakuchunia BARIDA mwanangu..!!

    Malubano ya Kiki hakuna tena muulize Jitto asaliu Ammri.

    Hii ni Tanzania ya Kaazi kwea mele.
    Dkt Bashiru amesha sema hakuna malumbano ni Wapuuzi WAPUUZENI.
    SEMBUSE WEWE UVUME KWA UPEPO GANI SISIMIZI.
    MUULIZE YNALANDU AMEESOMA ALAMA ZA NYAKATI.

    KAA CHONJO SAA MBAYA. UNA UHAKIKA UMEMALIZA DOZI NA VIDONGE VYAKO.
    POLE MWANA WANEE.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Swadakta mdau.
      Huyu Nchemba naona anapoteza Netweki ajili ya madawa mchanganyiko. Hatuumtaki tena
      kwanza hakuwa anatuwakilisha.
      alikuwa mtafuta Umaarufu na kiki Bungeni. HATUKUTAKI

      Delete
  2. Mbona kulio?
    umesha Maiza kuipaka Mtope nchi yetu!

    Mie nnavyojua mwenye kufanya hivyo huwa anajirahisishia suala lake la Ukimbizi. Auametolewa Nje. wazungu Nuksi. Hakuna kula vya Bure.

    NO FREE LUNCH. NJOO UMU OMBE
    MANYAMA KAMA ATAKUAJIRI OFISINI KWAKE.

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad