Aliyekuwa Mbunge wa Singida Mashariki (Chadema), Tundu Lissu, amesema yeye na timu yake wako tayari kutinga Mahakama Kuu muda wowote kuanzia leo maandalizi yote yanayohitajika yamekamilika.
Lissu aliyasema hayo kupitia akunti yake ya Twitter kuwa kesi za ubunge ni kesi za kisiasa. Ni kesi nyeti na zinahitajika umakini mkubwa katika kuziandaa na kuziendesha.
“Mimi na timu ya mawakili wangu tupo tayari kuingia Mahakama Kuu ya Tanzania. Tutafanya hivyo muda wowote kuanzia leo maandalizi yote yanayohitajika yamekamilika,” aliandika Lissu.
Lissu alieleza kuwa atawajulisha mara moja kesi hiyo itakaposajiliwa rasmi.
“Kama itawapendeza nitawaomba mtakaopata nafasi kuhudhuria mahakamani kwa niaba yangu wakati wowote kesi hiyo itakapokuwa inaendelea,” alieleza Lissu.
Kesi za ubunge ni kesi za kisiasa. Ni kesi nyeti na zinahitaji umakini mkubwa katika kuziandaa na kuziendesha.Kesi za ubunge ni kesi za kisiasa. Ni kesi nyeti na zinahitaji umakini mkubwa katika kuziandaa na kuziendesha.— Tundu Antiphas Lissu (@TunduALissu) July 31, 2019
Mimi na timu ya mawakili wangu tuko tayari kuingia Mahakama Kuu ya Tanzania. Tutafanya hivyo muda wowote kuanzia leo. Maandalizi yote yanayohitajika yamekamilika.
Mimi na timu ya mawakili wangu tuko tayari kuingia Mahakama Kuu ya Tanzania. Tutafanya hivyo muda wowote kuanzia leo. Maandalizi yote yanayohitajika yamekamilika.
Tundu Antiphas Lissu
@TunduALissu
Nitawajulisheni mara moja kesi hii itakaposajiliwa rasmi. Kama itawapendeza, nitawaomba mtakaopata nafasi kuhudhuria mahakamani, kwa niaba yangu, wakati wote kesi hiyo itakapokuwa inaendelea.
21
5:26 PM - Jul 31, 2019
Twitter Ads info and privacy
See Tundu Antiphas Lissu's other Tweets
AMEHITIMISHA KUTUMIA DAWA
Aidha, Lissu ameeleza kuhitimisha matumizi ya dawa alizoanza kutumia tangu Septemba 7 mwaka 2017 na sasa yupo tayari kurudi Tanzania September 7 mwaka huu.
Nimehitimisha matumizi ya dawa nilizoanza kuzitumia tangu Septemba 7, 2017. Sasa nipo tayari kurudi nyumbani September 7, 2019.
— Tundu Antiphas Lissu (@TunduALissu) July 31, 2019
Tundu anti pasi lizzu.
ReplyDeleteSalama...!!
Umesha sahaulika Jimboni na Nchini.
Sasa sijui anaekupa EA Taime in Nani?
Manake ukiwa Hamnzo hapa Kuna Vichaa Kabisa.
Kuwa na Adabu na Ikushike.
Ile Tanzania ya awamu ile ya wewe kuwa staa Mwachie Steve Nyelele
Wewe tafuta mtaji wa Pango uanzishe ofisi kama utapata leseni baada ya kukidhi vigezo umsaidie kibatali au Ludi singida ukalime Alizeti.. Soko ni Zuri na Bei inalipa.