UCHAMBUZI: Nani ana makosa, Ali Kiba na Fid Q au Harmonize?


Kwanza kabisa nianze kwa kusema sikuwa najiona kama nitaweza kuandika hii makala kwa mfumo wa Uzi huku jf. Ila kwa kuwa mimi, binafsi, ni shabiki wa sanaa haswa muziki na tukio hili linahusisha moja kwa moja muziki, basi sio shida nikamwaga wino kidogo.

Kabla sijaanza kuelezea chochote niweke jambo moja sawa kwamba; Uchambuzi wangu hauko sahihi kwa asilimia 100. Hii ni kwa sababu tukio lile halina 'dairekti eksiplanesheni.'

Ni kitu ambacho kukitolea ufafanuzi wa moja kwa moja itakuwa ni uongo kwa sababu tunafungwa na nadharia mbili.

Moja ikiwa ni, Labda ile ilikuwa coincidence. By the time Harmonize anaingia ni muda ambao Ally alikuwa amepanga kuondoka. Shida inakuja msafara ulionyanyuka na namna walivyonyanyuka kuongozana. Hapa kuna body languages na countenance. Na;

Mbili ikiwa ni, Labda ni maksudi kwa sababu binafsi za kifaida kwa wote. Yaani kibiashara na kwa mtu mmoja mmoja - Hapa naongelea usalama na kulinda 'brand' ya mtu husika.

Tukubali tukatae muziki wetu una mambo kibao. Sababu za wote kutoonesha ushirikiano wa salamu au kujali inaweza ikawa ni bora zaidi kuliko wangepeana hizo salamu. Hata hivyo, hawana mawasiliano. Kulikuwa na sababu ipi ya kusalimiana kama wengi mnavyotaka??? Hakuna kitu kibaya kama unafiki... I congratulate them for what they did. It doesn't matter how you define it.

Pia agenda ilikuwa kutoa pole kwa wafiwa. Najua ni msiba wa wote lakini naongelea the main victims - watu ambao msiba umewagusa moja kwa moja na Ally alifanya alichofanya, plus harmonize and even Fid Q.! Wote walitimiza lengo la kufika msibani na kutoa pole zao... What else did you want?? Si Agenda imeisha au??

Shida ni moja, humans choose to see what they want to see, to hear what they want to hear.! Hata kama unaeleza jambo kwa namna ambayo ni ukweli mtupu kuna watu wachache watakataa. Na ndivyo ilivyo!!

Wengi wetu au wote tumeiona ile video ikiwa na Kapsheni. Kwa mtazamo wangu, kuipa tafsiri nzuri, mtu angetakiwa kuiona bila ya kupewa maneno. Nadhani hapo ndio utakuwa na akili iliyo huru. In a subtle way the caption gave people a prejudiced opinion na uharaka wa kuitazama no one bothered to ask themselves whether or not to side with the caption.

Psychologically, chances are that, people arrived at conclusions exactly at the moment after they read the tittles and headings, not after they watched the video... Mpaka wanaitazama video tayari wanashika mtazamo fulani. Isingewezekana mtu kuuona ukweli.!!

Narudia tena, lengo la kwenda kwenye msiba ule ilikua kutoa pole kwa wafiwa, jambo ambalo, Harmonize, Fid Q, Ali na wanawe walilifanya. Hapo shida iko wapi??

Ni kama tu ukiwa unatazama muvi. Tuchukulie kisa cha wana wa Israel na fimbo ya Musa labda; Wakati wanavuka ule bahari. Somo kubwa ni kwamba kusonga mbele bila kusita na kwa imani lakini watu huwa wanachagua kuona kama Mussa ndiye shujaa wakati Mungu ndiye aliruhusu yote yafanyike. It's the same here.. Hatuoni kitu halisi baadala yake tunanogewa na jambo ambalo hata sio la msingi.

Na hapa ndio nawapata wale manangu wanaolia harmonize kuongozana na body guards msibani. Ebu muwache unafiki.

Kiwango cha usalama wa mtu anakifahamu mwenyewe... Hakuna anayejua jamaa anajikinga na nini?? Hakuna anayejua ana maadui wangapi. Ishu ya yeye kuwa na body guards kosa linakuwa nini??

Muda mwingine it's not show offs. Inamlazimu mtu kufanya hivyo. Dunia haieleweki hii... Taking precautions is necessary tena is a MUST. Keep it up my G. Ikiwezekana uwe unatembea na wanajeshi kabisa.

Tatizo sisi binadamu tunawahi kujaji bila kutaka kujua....

We choose to distort the reality of a situation so that it meets our perception.

Nikirudi kwenye mada kwa tukio hilo la msibani, kama ukiniuliza, nitakwambia hakuna mwenye makosa. They both did what we expected them to do - kuhudhuria msiba. Full stop!! Mengine hayo ni shauri zao

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad