Uchunguzi wa DNA wafanikishwa kutambulika kwa aliyesababisha vifo vya watu 20

Polisi nchini Misri siku ya jana  waligundua mshambuliaji aliyesababisha vifo vya takriban watu 20 kwa kutumia vilipuzi alivyokuwa ameviweka kwenye gari katika mji mkuu wa Misri Cairo mapema wiki hii.

Mwanaume huyo ambaye anajulikana kwa jina la Abdul Rahman Khaled Mahmoud ni wa kikundi chenye silaha cha Hasm kilichoshikamana na kikundi kilichopigwa marufuku cha 'Muslim Brotherhood'.

Utambulisho wa mshambuliaji huyo umethibitishwa baada ya kulinganisha DNA yake na wanafamilia, wizara ya mambo ya ndani ya Misri ilisema katika taarifa yake.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad