Ufafanuzi wa Polisi juu ya taarifa zilizoenea zikidai DC katekwa

 


Jeshi la Polisi Mkoani Mbeya wamekanusha taarifa ya kutekwa kwa DC wa Kyela Claudia Kitta pamoja na msafara wa Kamati ya Ulinzi na Usalama Wilaya, huku wakithibitisha msafara huo kushambuliwa kwa mawe walipofika kumuokoa Mama aliyetaka kuuawa na Wananchi akidaiwa kumuua Mwanae wa kumzaa.


“DC na wenzake wako salama hali ya amani na utulivu imerejea mimi nipo eneo la tukio, kuna Bwana amefariki kwenye uwanja wa mpira Wananchi wakawa wanahisi Mama yake Mzazi amemuua kwa imani za kishirikina, maiti ilipotaka kuzikwa wakakataa wakamtaka Mama yake amfufue”-POLISI MBEYA


“Kamati ya Ulinzi na Usalama wakiongozwa na DC wa Kyela walikuwa maeneo hayo katika ukaguzi wa mambo ya mwenge na mitihani, waliposikia taarifa za Mama kushambuliwa akidaiwa kumuua Mtoto wake, wakapita ili wajiridhishe, Wananchi wakafunga njia na kukazuka vurugu” – POLISI MBEYA


“Hakuna mtu ambaye amelazwa wala kujeruhiwa isipokuwa vurugu zilikuwa kubwa kidogo ila walijtahidi kutumia mbinu kujiokoa na sisi tuliwahi kufika na kuwasaidia, bado nipo hapa ili kufuatilia zaidi kujua waliohusika na vurugu hizo”– POLISI MBEYA


“UGUMU WA MAISHA NIKAAMBUKIZWA UKIMWI GEREZANI, NASUBIRI KIFO, NDUGU WOTE WAMEFARIKI”

 

 

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad