Uganda Yapata Kibali cha Kusafirisha Bangi Ulaya

Wakaguzi kutoka Umoja wa Ulaya (EU) wameidhinisha Uganda kutuma bidhaa za bangi barani Ulaya, gazeti la Daily Monitor linaripoti.

Bangi itakayotumwa kwenye soko la Ulaya hata hivyo si kwa matumizi ya starehe kama uvutaji bali ni kwa ajili ya matibabu.

Kwa mujibu wa Monitor mainspekta wa bidhaa za matibabu zitokanazo na bangi kutoka Uholanzi walikagua mashamba ya bangi kwenye wilaya za Hima na Kasese kati aya Julai 29 na Agosti 4.

Maafisa hao kabla ya kuondoka Uganda waliikabidhi cheti cha kukidhi vigezo kampuni ya Industrial Globus Uganda Ltd kwa kipindi cha Agosti 6, 2019 mpaka Agosti 5, 2020.

Vigezo gani vitawakutanisha Trump na Rouhani
Watanzania wauliza: 'Je tutajifunza kweli?'
Raia mwingine wa Rwanda auawa uhamishoni
Mkurugenzi wa kampuni hiyo, Benjamin Cadet amelithibitishia gazeti hilo kuwa EU wamewapa idhini ya kuasafirisha bangi Ulaya.

"Baada ya EU kuthibitisha bidhaa zetu - usafirishwaji na mnyororo wote wa uzalishaji - kuanzia kupanda mpaka kuvuna kwa bangi utafanyika kikamilifu nchini Uganda na kupelekwa kwenye masoko ya Ulaya," Cadet amesema.

Hakimiliki ya Picha @DailyMonitor@DAILYMONITOR
Takribani kampuni 50 zimeomba kibali Wizara ya Afya kuungana na kampuni ya Industrial Globus Uganda Ltd ili kuzalisha bangi kwa ajili ya matibabu.

Bangi inayozalishwa Uganda katika shamba la wilayani Kasese ina virutubisho vya Cannabinol (CBD) na Tetrahydrocannabinol (THC) ujazo wa 2.7mg THC na 2.5mg CBD mtawalia. Virutubisho hivyo vimepasishwa Ulaya, Marekani na Canada.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad